Jonas Mkude awekwa kando
Kiungo wa Simba Jonas Mkude ambaye
alikuwa Nohodha wa klabu hiyo leo amewekwa kando na kuwa mchezaji wa
kawaida wa Simba huku nafasi yake ikichukuliwa na beki wa Kimataifa raia
wa Zimbabwe Method Mwanjale.
Kiungo wa Simba, Jonas Mkude.
Mabadiliko
hayo ya Simba yametangazwa na Mkuu wa Idara ya Habari ya Simba, Haji
Manara na kusema kuwa benchi la fundi la klabu ya Simba chini ya Kocha
Mkuu Joseph Omog ndiyo wamefanya mabadiliko hayo wakiwa na lengo la
kuboresha kikosi hicho.
"Benchi la ufundi la klabu
ya Simba,chini ya kocha wake mkuu Joseph Omog limefanya marekebisho
kwenye eneo la unahodha wa timu. Katika marekebisho hayo yaliyoridhiwa
na uongozi wa klabu, beki wa kimataifa Mzimbabwe Method Mwanjale
ameteuliwa kuwa nahodha mpya wa timu ya Simba, akichukua nafasi ya Jonas
Mkude atakaendelea kuwa mchezaji mwandamizi kwenye kikosi" alisema Haji Manara
Aidha klabu hiyo ya Simba imefanya mabadiliko mengine kwa kuwateua
wachezaji bora wa Ligi Kuu ya Tanzania kuwa manahodha wasaidizi wa timu
hiyo.
"Kwenye mabadiliko hayo ya
kawaida, benchi la ufundi pia limewateua Mchezaji bora wa ligi kuu ya
Tanzania na klabu ya Simba kwa msimu huu, Mohammed Hussein(Tshabalala)
na John Raphael Boko kuwa manahodha wasaidizi wa timu hiyo." aliongeza Haji Manara
Klabu ya Simba ipo nchini Afrika Kusini kwa ajili ya maandalizi ya
msimu ujao wa Ligi Kuu bara 2017/2018 lakini kikosi hicho kinatarajiwa
kurejea nchini siku za karibuni kwa ajili ya bonanza la Simba Day ambalo
litafanyika tarehe 8 mwezi wa 8 mwaka huu.
No comments:
Post a Comment