Mwakyembe apigilia msumari TFF
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe amefunguka na kupigilia msumari
jambo ambalo linaendelea (TFF) na kusema ni muendelezo ya kampeni ya
serikali ya awamu ya tano kusafisha kila sehemu na kuleta uadilifu.
Mwakyembe
amesema serikali ya awamu ya tano imeamua kusafisha kila kona na
kufikia sehemu zingine ambazo zilikuwa haziguswi ndiyo maana kuna baadhi
ya viongozi wa michezo nchini wamefikishwa kwenye vyombo vya sheria kwa
hatua zaidi.
"Kama ni mabadiliko mimi
nimeridhika nayo tunakwenda mbele nimefurahi kwamba kulikuwa na vikwazo
viwili vitatu saizi vimeondoka tutafanya uchaguzi kama ilivyopangwa na
nina uhakika tutapata timu nzuri ya kuongoza mchezo wa soka nchini. Mimi
naomba Watanzania watuelewe kitu kimoja nchi nzima iko katika kampeni
ya kuondoa ubadhilifu, wizi, udokozi, rushwa katika maeneo yote,
haiwezekani tukawa na kakisiwa hapa Tanzania hakafikiwi, hakashikiki
wala hakaguswi ambapo kila mtu anajua nikiwa pale siguswi haiwezekani
hilo kwa serikali ya awamu ya tano" alisisitiza Mwakyembe
Mbali na hapo Mwakyembe aliendelea kusema kuwa kushirikiliwa kwa
baadhi ya viongozi wa TFF na vyombo vya dola si kwamba serikali
inampango wa viongozi hao kutogombea katika nafasi mbalimbali bali
serikali inafuata sheria hivyo hawawezi kusema jinai isubiri mpaka
uchanguzi ufanyike.
"Kinachoendelea sasa hivi ni
kampeni ya serikali kuhakikisha kuwa kunakuwa na uadilifu mkubwa katika
kila kitu ambacho tunakifanya, sasa hawa viongozi wa Simba wana
uchaguzi gani kesho? Hata kesho mtu mwingine yoyote ataingia humo mimi
sijawahi kuona hata simu moja sheria inayosema kama kuna uchaguzi basi
sheria ya jinai isimame mpaka uchaguzi ufanyike, hiyo mimi sijawahi
kuona. Kichanofanyika ni kampeni ya kawaida kabisa kuhakikisha katika
nchi yetu hakuna tena sehemu ambazo ndiyo uchafu unatupwa huko" alisisitiza Mwakyembe
Mbali na hilo Mwakyembe ameonyesha wasiwasi kuwa fedha ambazo
Watanzania walichanga kwa ajili ya timu yao ya Serengeti Boys ilifanyiwa
hujuma na kupigwa na baadhi ya viongozi wa soka na kusema kwa sasa wapo
kwenye mpango wa kufanya uchunguzi kubaini hilo na kujua ni wapi
walikosea mpaka pesa hizo zimeweza kupigwa na wajanja.
No comments:
Post a Comment