Trending News>>

Manula amvulia kofia Said..


Mlinda mlango wa Taifa Stars, Aisha Manula amefunguka ya moyoni kwa kumpongeza golikipa namba mbili wa timu hiyo Said Mohamed 'Nduda' na kudai anastahili kupewa pongezi kwa kuweza kukipa ushindi wa tatu kikosi hicho cha Stars.
Manula ametoa salamu hizo baada ya Nduda kuisaidia Taifa Stars usiku wa jana kuweza kushika nafasi ya tatu katika michuano ya COSAFA iliyofanyika nchini Afrika Kusini katika hatua ya penati baada ya kipa huyo kudaka mkwaju uliyopigwa na Nahodha wa Lesotho, Thapelo Mokhehle wakati penati nyingine iligonga mwamba na kupeleka Stars kuongoza kwa penati 4-2
"Hakika wewe ni bora 'brother' na mara zote umekuwa bora, kazi uliyoifanya ni kubwa mno kwetu watanzania. Unastahili kupewa pongezi kwa ulichofanya, kwangu mimi wewe ndiyo 'Man of the match' na unastahili 'brother keep it up'", ameandika Manura kupitia ukurasa wake wa Instagram.
Kutokana na ushindi huo, Tanzania inaondoka na dola za kimarekani 10,000 zaidi ya shilingi Milioni 22 kwa fedha za kitanzania wakati Lesotho wakiwa wamepata dola 8,300.
Kwa upande mwingine, fainali ya COSAFA 2017 zinatarajiwa kuendelea kuchezwa kesho kwa kuzikutanisha Zambia na Zimbabwe kwenye uwanja wa Royal Bafokeng, Phokeng mjini Rusternburg na atakayeweza kubahatika kuwa bingwa wa michuano hiyo ataweza kuondoka na Dola 42,000 huku mshindi wa pili kuchukua  Dola 21,000.

No comments:

Powered by Blogger.