Mume kufukuzwa kazi kumenifundisha kuchepuka, sasa nimekuwa sugu
Lakini tangu mwaka jana February mume wangu alipata matatizo kazini kazi ikawa imeisha, na mimi ni mama tu wa nyumbani, huwa saa nyingine nafanya vibiashara vidogo vidogo kwa msimu tena.
Sasa mwenzenu maisha yalinishinda, ilifikia point mwanaume anashinda ndani tu hatuna chochote cha kula na watoto, nikaona hakuna namna wacha niokoe jahazi kama mama. Kuna jamaa alikua ananimendea tangu kitambo sana nilikua sina mpango sababu mume alikua akinipa kila nilichotaka.
Naomba niseme hivi; NILICHELEWA KUCHEPUKA NA HUYU BWANA, maana mambo anayonipa sijawahi kupata. Mpaka sasa yeye ndio kanipa pesa nimelipa kodi ya nyumba, kanipa ada za wanangu, ananipa matumizi ya nyumbani, maisha safi, stress zote kwiiishhhhaaaa niko na tabasamu masaa yote.
Tumesisitizana kila mmoja aheshimu ndoa yake, nimemsisitiza sana asibadili mwenendo wake mbele ya mke wake na familia yake. Nami nimejiapiza kumuheshimu mume wangu mpaka mwisho, tunafanya kwa usiri mkubwa sana lakini kila mmoja wetu anapata raha ile mbaya.
No comments:
Post a Comment