Mshahara mpya wa Lionel Messi kufuru tupu
Mshambuliaji wa Barcelona, Lionel Messi.
LIONEL Messi amesaini mkataba mpya unaomfanya alipwe mshahara ambao
umevuka kiwango kinachotakiwa kulipwa kwa mchezaji, lakini Rais wa
Barcelona, Josep Maria Bartomeu, amesisitiza fowadi huyo anastahili
alipwe hivyo kwa kuwa ni mchezaji bora zaidi katika historia ya soka.Messi, analipwa pauni 500,000 (Sh bilioni 1.4) kwa wiki, katika mkataba wa miaka minne unaotarajiwa kumalizika mwaka 2021.
Rais huyo amepuuza uvumi kwamba mshahara huo unaweza kuwaletea matatizo Barcelona kutoka kwa Shirikisho la Soka Ulaya, kupitia kitengo chao cha Financial Fair Play.
BARCELONA, Hispania
No comments:
Post a Comment