MAHREZ AONYWA KUPIGWA CHINI LEICESTER
Mahrez aliitangazia Leicester kuwa anataka kuondoka katika kipindi hiki cha usajili, na Arsenal ndiyo klabu inayomuwania lakini haipo tayari kutoa kitita cha pauni milioni 50 ambacho Leicester wanataka.
“Suala la yeye kuondoka tunalijua lakini bado ana mkataba na klabu yetu. Tunatakiwa kuwa weledi kwake lakini zaidi anatakiwa kuonyesha kujituma, na nadhani anatakiwa kuwaonyesha mashabiki, viongozi na wachezaji kuhusu hilo. Kama akipangwa ni lazima aonyeshe juhudi na kama hataionyesha, hatacheza,” alisema Shakespeare.
No comments:
Post a Comment