MAMBO MUHIMU YA KUFANYA BAADA YA KUFUNGUA BLOG/WEBSITE
Baada
ya kufungua tovuti yako kuna mambo ya msingi na ya muhimu kuweza
kuyafanya na kuweza kuweka tovuti yako katika hali nzuri.Vile vile
kufanya hivi kutachangia katika kuboresha na kuongeza watembeleaji
katika tovuti yako;
Andika mada bora na kila baada ya muda fulani.
Mara baada ya kufungua tovuti yako hakikisha unaanda na kuandika mada
ambazo ni nzuri na bora.Andika mada zitakazovutia kusoma na zina hadhira
pana.Epuka kuandika mada ambazo zina hadhira ndogo maana hautopata
watembelewaji wa uhakika.Andika mada ambazo zinaendana na muda huu
(updated content)
Weka tovuti yako katika google/bing webmaster tools. kujiunga na bing bonyeza hapahttp://www.bing.com/toolbox/webmaster na kujiunga na google webmaster bonyeza hapahttps://www.google.com/webmasters/
Kwa kuweka tovuti yako katika hizi webmaster tools kutakuwezesha kujua
tovuti yako ina tatizo gani na uweze kulitatua kwa muda muafaka.kupitia
hizi webmaster tools utaweza kufanya mabadiliko yoyote kwenye url yako
na kuweka au kupunguza maneno katika search results.Ukitaka baadhi ya
url zako zisionekane katika serch results ni lazima upitie hapo katika
webtools.Vile vile utaweza kujua site yako kama ina malware au ipo under
attack.Hauwezi kujua tovuti yako vizuri mpaka upitie hapo katika
webtools.
Unganisha site yako na google analytics(au other free/paid analytics tools) kujiunga na google analytics bonyeza hapa https://analytics.google.com/
Kuunganisa site yako na analytics tools kutakuwezesha kujua idadi ya
watembeleaji katika tovuti yako kwa muda fulani.Utajua tabia ya
watembeleaji wako ,muda wanaochukua katika site yako ,sehemu wanapo
toka,jinsia, umri na vitu vingine vingi.Mjumuisho wa vitu hivi
vitakuwezesha kujua watembeleaji wako na kufanya marekebisho katika site
yako kuweza kuvutia watembeleaji wengi zaidi.
No comments:
Post a Comment