Jinsi ya kuficha Mafaili na vitu vyako Muhimu ndani ya Calculator kwenye Smartphone yako..
Kama ilivyozoeleka watu wengi tuna video, picha au vitu ambavyo tumeweka
kwenye smartphone zetu, ambavyo si vizuri vikaonekana kwa kila mtu.
Tatizo la smartphone ni kwamba kila mshikaji utaekutana nae juma au
saidi atataka aangalie muundo, uwezo, kamera na toleo lake. Na inakuwa
vigumu kuweza kumkatalia mtu hasa kama ni rafiki yako wa karibu sana.
Ukisema utengeneze folda ambalo linaonekana kwa urahisi halafu uweke
picha, video na faili zako za siri lazima watashitukia na kutambua
kilichomo ndani. Siku za nyuma , tulikuwa tunatengeneza folda halafu
tunaliandika 'virus' na kuweka vitu vya siri humo ili kumtisha mtu
asiweze kufungua kutokana na jina la folda hilo akizani ni kirusi kweli.
Ila siku hizi ujanja huu kila mtu anaujua. Wakati kukiwa na njia nyingi
tu za kuweza kuficha vitu vyako vya siri kwenye smartphone yako, leo
nitakuonesha namna ya kuficha vitu vyako vya siri katika App unayoitumia
kila siku ya Calculator.
Ndiyo, Calculator! kuna app inayoitwa 'Smart Hide Calculator' ambayo
unaweza ukaitumia kukokotoa mahesabu pia inaweza tumika kuficha vitu
vyako vya siri na muhimu kwa watu wadukuzi wa mambo. Smart Hide
Calculator ni app ambayo unaweza ukahifadhi picha, video na faili zako
muhimu kwa siri kwenye mgongo wa Calculator. Unachotakiwa ni kuweka
namba ya siri kisha unabonyeza sawa sawa '=' kisha vitu vyako
vitaonekana ndani ya app hiyo.
Fuata hatua zifuatazo kuweza kutumia app hiyo.
Hatua ya 1. Kwanza kabisa, pakua kisha ingiza app ya Smart Hide
Calculator kwenye Google Playstore au bonyeza link ifuatayo >> Pakua hapa Smart Hide Calculator
Pakua 'Smart Hide Calculator' Playstore
Hatua ya 2. Fungua App yako itakutaka uingize namba ya siri. Hakikisha
kuweka namba ya siri ambayo ni ngumu kwa mtu kuweza kuitambua na rahisi
kwa wewe kuikumbuka kwa sababu hiyo ndiyo itatumika kufungua na kufungia
vitu vyako vya siri ndani ya calculator hiyo.
Ingiza namba ya siri
Hatua ya 3. Baada ya kuhakiki namba ya siri, wewe na mtu yeyote
atakayefungua simu yako ataiona app hiyo kama calculator ya kawaida
kabisa.
Muonekano wa Calculator hiyo
Hatua ya 4. Ili kuingiza vitu vyako vya siri, unatakiwa kuingiza namba
yako ya siri kisha bonyeza kitufe cha sawa sawa '=' ili kufungua vitu
vya ndani.
Fungua vitu vyako vya ndani ya app hiyo
Hatua ya 5. Baada ya kufunguka ndani utaona mipangilio ya kuficha
mafaili (Hide Files), kuyaondoa mafichoni (Unhide Files), kubadili namba
ya siri (Change Password) nakadhalika.
Muonekano wa ndani wa app hiyo
Bonyeza kwenye 'Hide Files' kisha chagua mahali ulipo hifadhi vitu vyako kama video, picha, miziki au faili unazotaka kuzificha.
Chagua mahali ulipoweka vitu vyako
Bonyeza 'OK' kuficha vitu vyako muhimu ndani ya app inayoaminika
duniani, Calculator yako. Kama ukitaka kuyafichua mafaili yako fungua
hiyo Calculator kisha chagua 'Unhide Files' na faili zako zitakuwa nje
ya Calculator hiyo.
Bonyeza kwenye 'Unhide Files' kufichua vitu vyako
Kama ukisahau namba ya siri, usijali, unaweza ukairudisha namba yako ya siri kwa kuandika namba hizi 123456789+987654321
Namba ambazo zitakusaidia kama ukisahau namba yako ya siri
App ya Smart Hide Calculator kiufupi ni moja kati ya app nzuri kwa kuficha faili na vitu vyako muhimu kwenye smartphone yako.
No comments:
Post a Comment