JINSI YA KUENDESHA BLOG KWA KUTUMIA SIMU NA MAMBO YA KUZINGATIA
Kama unatamani kuwa na blog kuna mambo mawili nataka nikushirikishe leo:
1. Ni kweli unaweza kuendesha blog kupitia simu yako au tablet yako , na
tena kwa kutumia Play Store unaweza kuinstall app maalum ya blogger au
wordpress kutegemea na teknolojia gani unaitumia.
Kupitia apps hizo unaweza fanya mambo ya msingi kama kuandika post, na
kuedit post. Hata hivyo apps hizo si nzuri kama hauna kabisa blog. Mfano
kwa blogger inabidi kwanza uwe umetengeneza bog kwa kutumia browser
kama vile Google Chrome, au Firefox, kisha uitumie app kuandika, na
kuedit makala.
2. Utajiuliza kwanini nimetaja blogger na WordPress. Hizi ni teknolojia
zinazoongoza katika kutengeneza blogs. Zipo nyingine nyingi ila hizi
mbili ndizo zinazotumiwa na watu wengi zaidi. Mfano blog maalum ya
Tanzania ya MillarAyo imetengenezwa kwa kutumia WORDPRESS wakati blog ya
Issa Michuzi imetumia BLOGGER.
Kuna sababu za msingi na za kitaalamu kwanini mfano uamue WordPress badala ya blogger.
Blogger na WordPress zote ni bure, ila WordPress ambayo ni bure ina
vikwazo kadhaa mfano kuna kikomo cha kiasi cha uhifadhi unaoweza pata wa
picha na taarifa zako ukitumia wordpress.com , na hata kuziedit
templates zake kuna kikomo. Hata hivyo wordpress unaweza kuwa nayo na
kuihost mahali popote unapotaka wewe, tofauti na ilivyo blogger, ambayo
ni kweli ni bure kabisa, na haina ukomo wa kiwango cha uhifadhi -storage
capacity, ila huwezi ihamisha blog yako uipeleke kwa mtu mwingine.
WordPress hutupatia uhuru wa kutengeneza blogs na websites nzuri sana,
kwakutumia vitu vingine kama plugins na themes zilizo nzuri sana, hata
hivyo ifikapo kwenye swala la usalama , blogger ni kimbilio zaidi kwani
blogs za blogger zinasimamiwa na Google, hivyo usalama wake ni mkubwa
kuliko wewe binafsi kutafuta kampuni yoyote tuu ya kuhost blog yako ya
WordPress.
Usisahau RIYADI BHAI naweza kukusaidia kutimiza ndoto yako ya kuwa na
blog ya ukweli. Sio tuu kwamba tutaifanya blog yako ipendeze, ila pia
tutakuelimisha ujue vyanzo mbalimbali vya mapato ya blog ukiacha
matangazo, na namna ya wewe kunufaika binafsi ukiacha kifedha.
No comments:
Post a Comment