JINSI YA KUTUMIA FLASH DISK KAMA PASSWORD YA COMPUTER YAKO
Habari ni wakati mwingine tena leo ningependa kushare na nyie jinsi ya
kutumia flash yako kama ufunguo wa kompyuta yako au password,
Basi kwa kuanza basi ni vyema tukajua faida za kuwa na password katika flash drive,
kuwa na password kwenye flash drive hii ina kusaidia hasa pale unapokuwa
unasahau kwani tunakubaliana kuwa kuna wakati mtu unakua unasahau
password tena kuzingatia kwa sasa karibia kila kitu kinatumia password
kuanzia email mpaka simu yako ya mkononi hivyo basi ni rahisi sana kuwa
na kumbukumbu ya mahali ilipo flash yako zaidi ya kukumbuka password ya
kila kifaa unachotumia.
Pia ni rahisi sana kutumia kwani hakuna haja ya kutafuta sehemu ya
kuweka password bali unachokifanya ni kuchomeka flash yako tu basi hapo
utakua umepata uwezo wa kutumia kompyuta yako kirahisi kabisa.
Basi tukiwa tumesha jua hayo machache moja kwa moja twende tuka jifunze
namna ya kutumia flash drive kama password ya kuwasha kompyuta yako, ili
uweze kufanya haya unachohitaji ni flash na internet angalau MB100 ili
kuweza kupakua programu hiyo ya ku-wezesha kutumia flash kama password
ya kompyuta yako.
KUMBUKA : Huna haja ya ku-format flash yako bali hakikisha flash yako ina nafasi kidogo kama MB200 hivi au zaidi
Kwa kuanza basi cha kwanza bofya link hii hapa DOWNLOAD
kisha pakua programu ya predator na ufanye installation kwenye kompyuta
yako kumbuka kompyuta yako itaendelea kuwa on endapo flash yako itakuwa
imechomekwa kwenye kompyuta yako pale unapoitoa flash yako kompyuta
yako huzima moja kwa moja na kuonyesha ishara ya kuwa mtumiaji hana
uwezo wa kutumia kompyuta hiyo.
Basi ukisha pakua programu hiyo install kwenye kompyuta yako baada ya
hapo chomeka flash yako pale programu itakapo hitaji, kisha chagua
password yako na kisha bofya save. Hapo utakuwa umefanikiwa kuweka
password kwenye kompyuta yako kwa kutumia flash.
Ukisha maliza vyote hivyo kama imetokea unataka ku unstall programu hii
hakikisha flash inakuwa imechomekwa katika mashine yako kisha ndo uondoe
programu hiyo kwenye kompyuta yako.
Kama umependa hii unaweza kushare na marafiki na kama unataka mafunzo
zaidi kuhusu tech tembelea mtandao huu kila siku ili kujifunza mambo
mengine mengi yanayohusu teknolojia.
No comments:
Post a Comment