JINSI YA KUJIUNGA NA SEEBAIT NA KUJIPATIA KIPATO KUPITIA BLOG/WEBSITE
Habari ndugu zangu katika tech leo tutazungumzia kuhusu kujiinua
kiuchumi sisi kama blogger's, nalizungumzia hili baada ya kupata maswali
na maoni kuhusu seebait kutoka kwa blogger's wenzangu hivyo tunatimiza
Ahadi kama kawaida yetu, naam nisikupotezee wakati twende kwenye mada
moja kwa moja.
Jinsi ya kujiunga na seebait hatua kwa hatua hatua ya kwanza ingia kwenye site ya Seebait.com kisha bonyeza sehemu iliyoandikwa Login/SignUp
Itaonekana muonekano kama huu pichani
Itakuletea muonekano huo pichani , kwasababu sisi ndio tunahitaji
kujipatia pesa kupitia Seebait.com basi tutaenda sehemu iliyoandikwa
Select option you want to use kisha chagua mtandao unaohitaji kujisajili
seebait kupitia mtandao ulioidhinishwa na seebai ambao ni Facebook,
twitter na google+ hivyo nitakuonyesha kupitia google+ kwasababu
bloggers wengi tunatumia google+
ukibonyeza google+ itakuomba idhini hivyo bonyeza Allow,
Itakuwezesha kuingia katika dashibodi ya seebait kama inavyoonekana
pichani kisha utucopy hizo code na kwenda kuzipaste kwenye blog yako
Katika dashidadi ya seebait walishakuelekeza sehemu ya kuweka , hivyo
ingia kwenye blog yako bonyeza theme kisha edit Html, kisha search
maneno haya <head> [ jinsi ya kutafuta code kwenye HTML bonyeza
mouse yako mara moja kwenye code za templete yako kisha bonyeza Ctrl+F
utaona sehemu ya kusearch] kisha paste code za seebait chini ya code
hii <head>. save tempalte yako.
kisha rudi kwenye website ya seebait.com bonyeza sehemu inayosomeka Properties , kisha bonyeza Add Property
Utaona fomu kama hiyo hapo juu pichani jaza fomu hiyo kama hapa chini pichani
Hiyo picha hapo juu ni mfano hivyo jaza kutokana na mahitaji ya blog yako hakikisha hauvunji sheria zaseebait.com, kisha ukimaliza bonyeza Submit
Ukisha submit itakuletea muonekano huo hapo juu kama umekidhi mahitaji
ya seebait , lakini kuna vitu vitapungua kutokana na picha yangu ipo
aproved lakini yako haitakuwa aproved kwasababu bado hajakubaliwa na
kwenye status itakuonyesha not verify hivyo tumalizie hivi bonyeza
sehemu yenye alama ya mshale ulioelekea chini unapatinaka upande wa
kulia wa properties yako , utaidownload properties yako kupitia mshale
huo, kisha ifungue kwa ku doble-click , itafunguka kupitia browser yako
mimi nimetumia Chrome pichani hapa chini
Utaona code mfano wa hizo hapo juu sasa andaa code zako kwaajili ya ku
verify akaunti yako ya seebait , pia seebait wameelekeza kuhusu
kukamilisha hilo nenda juu kabisa kulia kwenye dashibodi ya seebait
utaona alama ya magazine bonyeza hapo kisha tafuta Property Activation
Utaona makala hiyo ya msaada wako imekuwa nambari moja bonyeza neno Read
itafunguka makala kisha copy code hii <meta name="seebait"
content="ACTIVATION CODE HERE" /> Kisha paste sehemu unayodhani
utaweza kuiedit mimi huwa natumia notepad kisha irekebishe hapo kwenye
neno ACTIVATION CODE HERE paste zile code za kwenye file ulilodownload
kwenye properties hivyo code zako zitakuwa hivi <meta name="seebait"
content="ryyady-bhay49d26e96ac7ebfc7c9t.html" /> Chukua code zako
hizo ulizozitengeneza vema kisha nenda kapaste chini ya kwenye code hii
<head> hii tulishazungumzia sehemu ya kuipata kwenye maelezo yetu
hapo juu.
kisha rudi tena kwenye dashibodi ya seebait.com nenda kwenye properties kulia bonyeza alama ya TIKI au Nike utaona mabadiliko sehemu ya status itaandika Active.
kufikia hapo umefanikiwa kuwa na akaunti ya seebait malizia kuweka matangazo kisha subiri seebait.comwaipitie fomu yako ya maombi kama umekamilisha utakuta notification kwenye dashibodi yako yaseebait.com
Mpaka hapo utakuwa umefanikiwa sasa jitahidi kutafuta Traffic kwa nguvu ili upate pesa zaidi
Kidokezo
Jinsi ya kuweka tangazo ingia kwenye dashbbodi ya seebait kisha bonyeza Ad Spaces kisha bonyeza Add Ad Space
Andika jina la tangazo, kwenye category chagua ukubwa unao uhitaji kisha bonyeza submit
kisha copy code sehemu iliyoandikwa space code kisha ka paste sehemu
unayotaka tangazo lako lionekane kwenye blog yako. HONGERA UMEFANIKIWA
Bila shaka umefanikiwa kama umezingatia vema maelezo hayo, lakini kama
hujaelewa usisite kuniachia maoni yako hapo chini wapi hujaelewa nami
nitakusaidia haraka iwezekanavyo, maoni yako sio lazima yawe kuhusu
swali kama umeelewa unaweza kuacha mtazamo wako hapo chini maoni yote
ninayapenda muhimu usitumie lugha chafu. sambaza makala hii kwa marafiki
ili tupate mwangaza wa mafanikio pamoja karibu sana
1 comment:
Kaka mbona umeiba makala yangu hujafuta sheria za copyright
Post a Comment