Makamu wa Rais apaa kuelekea Ethiopia kuhudhuria mkutano wa 29 wa AU
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan
ameondoka nchini jana jioni kuelekea Addis Ababa, Ethiopia ambapo
atahudhuria Mkutano wa 29 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa
Afrika (AU).
Katika
uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam,
Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan aliagwa na Viongozi mbalimbali
wa Serikali.
Katika
Mkutano huo wa siku mbili kuanzia tarehe 03-hadi 04 Julai-2017, Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan
atamuakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe
Magufuli kwenye mkutano huo.
Kabla
ya ufunguzi rasmi, Mkutano huo ulitanguliwa na vikao vya Baraza la
Utendaji linalowashirikisha Mawaziri wa Mambo ya Nje na Kamati ya
Uwakilishi wa Kudumu inayowahusisha Makatibu Wakuu wa Wizara za Mambo
ya Nje kutoka nchi Wanachama wa Umoja wa Afrika.
Mkutano
huo wa Wakuu wa Nchi na Serikali utafunguliwa rasmi leo tarehe
03-Julai-2017 katika Makao Makuu ya Umoja wa Afrika Jijini Addis Ababa,
Ethiopia na utajikita katika kujadili masuala mbalimbali yanayohusu
umoja huo.
Miongoni
mwa mambo yatakayojadiliwa katika Mkutano huo ni pamoja na taarifa
kuhusu Maboresho katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na
maboresho ya kitaasisi katika AU na hali ya Ulinzi na Usalama katika
bara la Afrika.
Kuhusu
hali ya ulinzi na usalama katika Bara la Afrika majadiliano ya
Viongozi hao yatajikita zaidi kwenye nchi za Sudan Kusini, Burundi,
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo- DRC na Libya. Aidha, majadiliano hayo
pia yatagusa hali ya usalama kwenye baadhi ya nchi ambazo ziliathiriwa
na kundi la Boko Haram za Nigeria, Niger, Chad na Cameroon.
Mkutano
huo 29 wa AU, unatarajiwa kuhuduhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres na Rais wa Mamlaka ya
Palestina Mahmoud Abbas.
Mkutano
huo 29 wa AU utakaofanyika Jijini Addis Ababa, Ethiopia utaongozwa na
Mheshimiwa Alpha Conde Rais wa Jamhuri ya Guinea ambaye ndiye
Mwenyekiti wa AU.
Kauli
Mbiu ya Mkutano huo ni Kuimarisha Mgawanyiko wa Idadi ya Watu Kupitia
Uwekezaji katika Vijana (Harnessing Demographic Divident Through
Investments in the Youth)
Imetolewa na Ofisi ya Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
ADDIS ABABA- ETHIOPIA.
No comments:
Post a Comment