JINSI YA KUWEKA MATANGAZO YA ADSENSE KATIKA BLOG YA KISWAHILI
Kwa Hali ya Sasa Kumekuwa na Blogs nyingi za Kiswahili ambazo mbali na
kujitahidi kupata Akaunti za Adsense bado wanakabiliwa na Changamoto
Kubwa ya Matangazo yao Kutooneka, Hii Inatokana na Google Adsense Kuto
Support Lugha yetu ya Kiswahili katika Kuratibu Uonekanaji wa Matangazo
katika Site Husika.
Leo Nitakupa Mbinu ambayo Itakufanya Ads ziendelee Kuonekana Japo Una
Tumia Lugha ya Kiswahili katika Blog Yako. Binafsi sio Mtaalamu sana wa
Mambo ya Codes, Ila nimekubali kujifunza na kujisomesha mtandaoni kwa
kadri ya Uwezo wangu. Hivyo Nitakuomba Uridhike na hiki kidogo
nitakachokupa leo nawe usisite kuitafuta elimu ya kujazia Sehemu
Nyingine kwani ELIMU HAINA MWISHO.
Japo kuwa sio lazima ujifunze kila kitu Tukirudi katika Mada yetu, Hatua
za Kufuata ili Matangazo yaweze Kutokea Katika Site za Lugha ya
Kiswahili:-
1. Ingia kwenye Dashboard yako ya Blogger, Nenda Mpaka kwenye Template, Click Customize Ili Ikupeleke kwenye Edit Css
Baada ya Hapo Nenda Kwenye Tab ya Advanced halafu Add CSS, Hapo
Utaingiza Codes za Design Hii kisha Una Apply to Template Halafu Unarudi
Kwenye Blogger Template Tena.
Weka Codes Hizi za Rangi Nyekundu
{ </script> google_language = "en";</script>
<meta content='Engish' name='language'/> }
hapo Juu.
2. Hatua ya Pili Unaenda kwenye Blog Dashboard yake unaingia Template
halafu Unabonyeza Edit HTML, Ikifunguka Bonyeza mouse yako kwenye code
za template kisha bonyeza CTRL+F (Amri ya Kutafuta) Ndani ya Kibox cha
Kulia Juu kwenye Codes za HTML utaingiza Codes Hizi <head> halafu
Bonyeza Enter. Chini ya Head Utaingiza Codes Hizi Hapa { <meta content='Engish' name='language'/> } Kisha Una Save.
Nia Na Madhumuni ni Kuilazimisha Site Yako Kwenye Meta Tags Iitambulishe
Kama Ni Site.Blog inayotumia Lugha ya Kiingereza. N.B.Unaweza Ukaweka
Mara nying hii Meta Tag kwenye Blog yako though Mimi nakushauri
Usizidishe mara 3.
3. Hatua ya Tatu ni Kuandaa Page ya Privacy Policy.
Hapa Utaenda Kwenye Dashboard yako Kisha Utaingia Sehemu ya Pages, Uta
Create Page ya Privacy Policy Kisha Utaandika Maneno angalau Paragraphs 4
kuhusiana na Site yako na Vile Ambavyo hautohusika n Comments mbaya
kutoka kwako au Wasomoaji wako, Kisha Unai Publish.
Ukishai Publish Unaenda Kwenye Layout katika Dashboard yako Ili Uchague
wapi Itakaa Hiyo Page ya Privacy Policy, Ingawa Ikakaa Juu Ni Bora
Zaidi.
N.B Post za Nyuma kabla ya Kufanya Trick Hii zinaweza Zisioneshe Ads
bali zitaanza Kuonesha zile zitakazokuja baada ya Trick Hii.
Kama Njia Hii Haitaleta Mafanikio Kwako, Ingia Kwenye Ku Edit HTML tena,
Kisha Tafuta data:post.body, halafu tafuta Post Footer au Post Footer
Line 1 Kisha Uingize yale maneno ya Privacy Policy Humo.
Thanks kwa Kuwa Nami, Kwa Maoni na Ushauri Usisite Kuwasiliana
Nami.Niachie maoni yako hapo chini nami nitayafanyia kazi kwa kukupa
majibu kadri nitakavyofahamu maswali yako.
1 comment:
ahsante sana mkuu
Post a Comment