Fahamu Matumizi ya Overdrive (OD) Kwenye Magari ya Automatic
Overdrive (OD) ni gia katika mfumo wa gari ambayo huifanya gari kuwa
katika spidi kubwa huku mzunguko wa injini ukiwa mdogo. Kwa lugha
rahisi, OD ni gia ya mwisho inayokupa mwendokasi. OD hukupa mwendo wa
kasi, uliotulia lakini kwa mzunguko mdogo wa injini (revolutions per
minute rpm). Hii hukuwezesha kuwa na matumizi madogo ya mafuta pengine
kwa kasi zaidi.
Overdrive ni kama gia ya ziada inayokupa mizunguko mingi ya driving
shaft kwa mizunguko michache ya injini yako. Unapaswa kuitumia ukiwa
unatembea mwendo mkubwa. Faida zake utatumia mafuta kidogo, maana gari
inakwenda kasi kwa mizunguko michache ya injini.
Mfano katika gari ya kawaida yaani 180km/h ili ufikishe spidi 120 basi
RPM inaweza ikawa 4000rpm katika barabara ya tambarare. Lakini ukiweka
overdrive unaweza kutembea spidi hiyo hiyo kwa rpm 2000 katika barabara
ya tambarare.
Utatambuaje kama Overdreive (OD) ipo on au off?
Pindi uonapo kitaa cha overdrive kwenye dashboard ya gari yako,
inamaanisha kuwa overdrive ipo off na pindi kitaa hicho kisipoonekana
basi tambua kuwa overdrive ipo on. Overdrive imewekwa kama chaguo
(option) la kutumia wakati ukiwa unatembelea spidi chini ya 60km/h.
Unaweza kutumia ukiwa unataka kuipita gari nyingine, mathalani kwenye
milima ambapo gari yako inakuwa imepunguza nguvu, hivyo unaweza kuiweka
off (hapa unakuwa kama umerudisha namba 4) na injini itabadili kasi ya
mzunguko, utaiweka ukishamaliza tena matumizi yake.
Eneo lingine, ni mara gurudumu la gari lako linapopasuka. Ikitokea
hivyo, unaweza kuondoa OD, huku ukiwa umeacha kukanyaga pedeli ya
mafuta, kwa maana ndiyo utakuwa unaomba mwendo upungue pasi na kukanyaga
breki. Katika hali kama hii, utakuwa umesaidia kupunguza mwendo wa gari
wakati ukithibiti muelekeo wa gari pia.
Katika hali kama hii huwa wanakanyaga breki. Kufanya hivi ni hatari,
maana unasimamisha kabisa mwendo wa gurudumu lililopasuka, na matokeo
yake mwendo wa gari, badala ya kwenda mbele, itajaribu kutii amri ya
gurudumu linalogomea gari kwenda mbele na kuamua kwenda upande wa
gurudumu lililopasuka, nikiwa na maana kwamba hapo gari itakuwa inaacha
njia na au kupinduka.
Kwa giaboksi zenye kujibadili zenyewe, ni vema basi tukaziacha OD
zijiendeshe zenyewe, maana kuziondoa hatari yake ni kuwa unaweza kusahau
kuiweka tena unapokwenda zaidi ya km 70 kwa saa, mfano barabara ya
Nyerere, na kusababisha matumizi makubwa ya nishati ya kuendeshea
mtambo.
Kitaa cha Overdrive kikiwa hakionekani kwenye dashboard yako maana yake
Overdrive ipo Automatic au on na hivyo ndivyo inavopendekezwa na
wataalam gari iwe automatic pindi upo mjini na unatembelea speed tofauti
(sometimes less or more than 60)..kwa vile overdrive inatumia gia kubwa
na mwendokasi chini ya 60km kwahiyo unaweza kutumia wakati unashuka
milima mikubwa.
-Mwananchi
No comments:
Post a Comment