WAZIRI MWIGULU NCHEMBA AWAPA ONYO KALI WANAOPINGA KAULI YA RAIS KUHUSU MIMBA KWA WANAFUNZI
Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba amezionya taasisi zisizo za
Serikali zinazohamasisha kudai haki ya mtoto anayepata mimba kurejeshwa
shuleni kuacha mara moja na zikiendelea atazifutia usajili.
Mwigulu ameyasema hayo leo, Jumapili wakati alipomwakilisha Waziri Mkuu,
Kassim Majaliwa katika harambee ya kuchangia ujenzi wa Parokia ya
Kisasa Mjini hapa.
Amesema Serikali haitaomba ushauri wala maoni kwa sababu maelezo yaliyotolewa na Rais, John Magufuli ni maagizo ya Serikali.
Waziri huyo amesema Serikali imetoa haki ya kila mtoto kupata elimu kwa
kuifanya kuwa bure kwa hiyo atakayeikosa asitafute kisingizio.
"Rais ametoa haki hiyo sasa hivi elimu ni bure, halipi tuition wala
nini, atakayeamua kuachana na haki hiyo asitafute kisingizio, asipeleke
lawama kwa Serikali, "amesema.
Chanzo-Mwananchi
No comments:
Post a Comment