Baraza la wawakilishi Zanzibar lataka adhabu ya ubakaji iongezwe
Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar wamesema adhabu ya kifungo cha
miaka 30 kwa watuhumiwa wa kesi za ubakaji imepitwa na wakati.
Wajumbe hao wamesema ipo haja ya kubadilisha adhabu hiyo kwa kuwekwa adhabu kali zaidi ili kupunguza wimbi la kushamiri kwa vitendo hivyo visiwani humu.
Mwenyekiti wa Kamati ya Wanawake na Watoto ya Baraza la Wawakilishi, Ali Suleiman Shihata amesema adhabu ya kifungo cha miaka 30 haiendani kabisa na athari ya tendo la ubakaji kwa sababu mtoto anayefanyiwa kitendo hicho huathirika kisaikolojia, kiakili na kimwili kwa muda mrefu katika maisha yake.
Shihata amesema licha ya kuwekwa kwa adhabu hiyo ya kifungo cha miaka 30, Mahakama za Zanzibar zimekuwa hazitowi adhabu hiyo na kesi nyingi za ubakaji zimekuwa zikitolewa hukumu adhabu ndogo ya chini ya miaka saba au mtuhumiwa kuachiwa huru.
Shihata ambaye pia ni Mwakilishi wa Jimbo la Kijitoupele, amesema kesi hizo zimeingiliwa na rushwa na ndio maana wabakaji wamekuwa wakiachiwa huru na kujigamba mitaani.
“Uwezo wa kifedha unaathiri sana kesi hizi za ubakaji kwa sababu rushwa imetawala kila mahala,lakini pia jamii bado imekuwa na ugumu kutoa ushahidi mahakamani,”amesema.
Mwenyikiti wa Kamati ya Ustawi wa Jamii ya Baraza la Wawakilishi, Dk Mwinyihaji Makame amesema jambo linalokera ni kesi za udhalilishaji kuchukuwa muda mrefu mahamakani hali ambayo imekuwa ikiwavunja moyo wanajamii hasa wathirika wa kesi hizo.
Kwa upande wao wajumbe wa asasi za kiraia zinazotetea haki za wanawake na watoto ambao ndio waandaaji wa mkutano huo, walipendekeza kuwa sheria zifanyiwe marekebisho hasa sheria ya mwenendo wa kesi za jinai ili iwe kisheria kesi za ukatili dhidi ya watoto kuwa ni miongoni mwa kesi ambazo hazina dhamana.
Akiwasilisha mapendekezo hayo kwa niaba ya asasi hizo, Dk Mzuri Issa Mkurugenzi wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (Tamwa) kwa upande wa Zanzibar, amesema ni vyema wajumbe wa baraza la wawakilishi, wanaharakati na mashirika ya kijamii kukutana kabla ya kuwasilishwa marekebisho ya sheria hasa yanayohusu masuala ya watoto na jinsia.
Miongoni mwa asasi zilizoandaa mkutano huo ni pamoja na Tamwa, Chama cha Wanasheria Wanawake Zanzibar (Zafela) na Kituo cha Huduma za Sheria (ZLSC).

No comments:
Post a Comment