VIDEO : Snura awakanya wasanii
Muimbaji na muigizaji bongo, Snura
Mushi amewakanya vijana wanaotaka kuingia katika tasnia ya sanaa
waepukane na vishawishi vya kujihusisha na matumizi ya dawa za kulevya
huku akidai kufanya hivyo hakufanyi uonekane unaenda na wakati.
Mwanamuziki Snura Mushi
Snura
amebainisha hayo kupitia kipindi cha eNewz baada ya kutuhumiwa
akijihusisha na matumizi ya dawa za kulevya ambazo zinamfanya kumpa
mizuko ya kufanya vizuri pindi akiwa stejini akitumbuiza.
"Vijana wenzangu kama
mnaingia kwenye sanaa achaneni na vishawishi, kuna vishawishi vya
kipumbavu sana, eti uonekane unaenda na wakati na ndiyo vinawaponza watu
wanaingia kwenye dawa za kulevya huko wanavuta bangi eti mtu apate
stimu afanye kazi vizuri nani kakwambia ?, mimi napanda kwenye steji
situmii kilevi cha aina yeyote Mungu wangu aliyekuwa mbinguni ni shahidi
sinywi pombe sivuti na nina panda kwenye steji nafanya vizuri tu kiasi
kwamba wewe unaweza kufikiri nimetumia kilevi kwa sababu akili yangu
nimeijenga kwamba hii ni kazi" alisema Snura
Mtazame hapa anavyofunguka zaidi
No comments:
Post a Comment