Trending News>>

SIMANZI:: Uongozi wa Yanga SC Wathibitisha Kifo cha Shabiki Ally Yanga


Kufautia kuzagaa kwa Taarifa ya kifo cha shabiki wa Dar young African mtandaoni mchana wa leo kilichotokea huko Mpwapwa Mkoani Dodoma.
Hatimae Uongozi wa Klabu ya Yanga umetoa taarifa rasmi ambayo imechapishwa kupitia ukurasa wa Facebook wa page ya Naipenda yanga na kueleza kuwa:-
Uongozi wa Yanga SC umepokea kwa masikitiko taarifa ya kifo cha Ally Yanga, hakika MUNGU ni mwema , faraja ya MUNGU wetu ikawe kwa familia katika kipindi chote cha majonzi kwa kuondokewa na mpendwa wao, Pia nasi Yanga kifo chake kina acha pengo kubwa kwa nafasi yake ambayo ilipelekea kujipatia umaarufu mkubwa na alikuwa balozi mzuri kama mwanachama na shabiki mkubwa wa timu yetu, Bwana alitoa, Bwana ametwaa.
Imetolewa na Idara ya Habarai na mawasiliano. Young Africans Sports Club. 20-6-2017.

No comments:

Powered by Blogger.