Trending News>>

Ukikutwa umevaa jezi ya Barcelona Saudi Arabia unapigwa faini ya pound 120,000 na jela miaka 15


Inawezekana ukashitushwa na taarifa hizi lakini ndio habari zilizoripotiwa na mtandao wa dailymail.co.uk wa England kuwa jezi ya FC Barcelona imefungiwa nchini Saudi Arabia na ukikutwa umevaa unaweza kufungwa.

Imeripotiwa jezi ya FC Barcelona yenye nembo ya Qarar Airways imefungiwa kuvaliwa na watu Saudi Arabia na ikitokea umevaa unaweza kupigwa faini ya pound 120,000 ambazo ni zaidi ya Tsh milioni 300 na kifungo cha miaka 15 jela.

Jezi za Barcelona ambazo zina logo ya Qatar Airways ambao wamekuwa wadhamini wao katika kipindi cha miaka minne iliyopita, Saudi Arabia inaripotiwa kuwa logo ya Qatar Airways ipo nje kisheria au kinyume na taratibu, hivyo ukikutwa utakutana na adhabu ya kifungo.

Good news ni kuwa FC Barcelona kuanzia msimu ujao wa 2017/18 wataanza kuvaa jezi zikiwa na mdhamini wao mpya Rakuten na sio Qatar Airways tena, hivyo mashabiki wa FC Barcelona nchini Saudi Arabia watakuwa na nafasi ya kuvaa jezi za timu yao zenye logo ya Rakuten na sio ya Qatar Airways.

No comments:

Powered by Blogger.