Siwezi kumkimbia Roma - Moni
Msanii anayewakilisha kanda
ya kati, Moni Centrozone ametoa ya moyoni kamwe hawezi kumtenga msanii
Roma kwa sababu alipata matatizo hivi karibuni kwani ni mtu aliyemshika
mkono kwenye 'game' ya bongo fleva.
Moni
kupitia kamera za eNewz amejibu tetesi za watu wanaodai kwamba
amejiweka mbali na msanii Roma tangu walipopata matatizo ya kutekwa na
watu wasiojulikana kwa siku tatu kwa kujibu siyo kweli kwani wao ni zidi
ya marafiki hivyo ni vigumu kutengana.
"Roma ni damu yangu, ni kaka
yangu ambapo kama siyo yeye nisingefika mapema kwenye 'mainstream' n
amaanisha ningechelewa kujulikana. Hata siku moja sijawi kufikiria
kujitenga naye kwa sababu yeye kapata matatizo. Mimi nimetoa ngoma kwa
sababu natakiwa kutoa na yeye bado anasubiri apone vizuri arudi kazini
kwani bado tuna kazi nyingi za kufanya muda mfupi tuu baada ya
kurejeshwa kwa studio ya Tongwe" - Moni alielezea.
Moni kwa sasa ana-'hit' na wimbo
unaokwenda kwa jina la tunaishi nao alioutoa muda mfupi baada ya kurejea
uraiani tangu alipotekwa na watu wasiojulikana akiwepo yeye, Roma na
Prodyuza Bin Laden na msaidizi wa ndani.
No comments:
Post a Comment