Dereva pikipiki achinjwa kwa Panga
Mwanaume mmoja (30) mkazi wa
Nyankumbu wilayani Nyamagana mkoani Geita anashikiliwa na jeshi la
polisi kwa kosa la mauaji ya dereva bodaboda yaliyotokea majira ya 3:00
Usiku tarehe 06.05.2017.
Kaimu
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza ACP Zarau Mpangule amemtaja mtuhumiwa
huyo kuwa ni Andrea anayedaiwa kupora pikipiki na kumuua dereva wa
pikipiki Bw. Alphonce Sekagi (32) mkazi wa wilayani Sengerema
wakilishirikiana na wenzake wawili kisha kutoroka na pikipiki
kusikojulikana.
Taarifa zinaeleza kuwa marehemu alikuwa dereva bodaboda wa mji wa Sengerema na siku ya tukio alipakia abiria watatu kwenye pikipiki yake wakitokea Sengerema mjini kwenda kijiji cha Tabaruka na kwamba wakati wakiwa njiani abiria hao walimkata dereva huyo na kitu chenye ncha kali shingoni kisha wakamchinja kwa kutumia panga shingoni na kupelekea kupoteza maisha papo hapo.
Kamanda Mpangule amesema wananchi walitoa taarifa polisi kuhusiana na tukio hilo ambapo askari walifanya ufuatiliaji wa haraka hadi eneo la tukio na kufanya msako mkali wa kuwatafuta watuhumiwa wa mauaji hayo katika maeneo mbalimbali kwa kushirikiana na wananchi ndipo jana tarehe 01.06.2017 majira ya saa 8:30 mchana wakafanikiwa kumtamata mtuhumiwa mmoja akiwa na pikipiki waliyoipora katika mauaji hayo.
Kamanda Mpangule ameendelea kwa kusema upelelezi na msako wa kuwatafuta watuhumiwa wengine wawili ambapo wanadaiwa kushiriki katika mauji hayo pamoja na uporaji unaendelea huku mtuhumiwa aliyekamatwa anafanyiwa mahojiano na uchunguzi ukikamilika atapandishwa mahakamani.

No comments:
Post a Comment