Trending News>>

Timu ya Kombaini ya Mjini Kukipiga na Jangombe Boys.


Na: Abubakar Khatib Kisandu, Zanzibar.

Timu ya Kombain ya Wilaya ya Mjini inatarajia kucheza mchezo wa kirafiki na Jang'ombe Boys kesho kutwa Jumatano saa 3 za usiku katika uwanja wa Amaan.

Kiingilio cha mchezo huo ni Shilingi Elfu moja na V.I.P ni shilingi Elfu mbili.

Kombain ya Mjini wanajiandaa na Mashindano ya Rolling Stone yanayotarajiwa kuanza July 9 hadi July 19, 2017 huko Mburu Manyara wakati Jang'ombe boys wanajiandaa na kuendelea kucheza hatua ya 8 bora ligi kuu soka ya Zanzibar.
Powered by Blogger.