Msuva amlilia Niyonzima
Mshambuliaji wa Yanga SC Simon Msuva
amesema japo kiungo Haruna Niyonzima ameacha pengo ndani ya timu,
wachezaji waliobaki wataendelea kuipigana kwa juhudi ili kuziba huku
mashabiki wakiamini hakuna pengo linaloonekana.
Simon Msuva na Haruna Niyonzima
Msuva
amesema, kuondoka kwa Haruna kumemuachia pengo kubwa ndani ya Yanga
kutokana na ushirikiano waliokuwa nao ndani na nje ya Timu lakini
atajitahidi kuendeleza ushirikiano na wachezaji waliobakia ili
kuhakikisha timu inaendelea kufanya vizuri.
“Katika timu lazima kuwe na
mazoea, mimi Haruna nilimzoea kupitiliza na hii habari kuwa amesaini
Simba SC mimi sifahamu lakini kwaupande wangu kama amesaini kweli mimi
nimeumia lakini ni maisha yake yeye na familia yake lakini mimi kwa
upande wangu nitajitahidi kwa sababu kuna watu wengine nipo nao pale
kama wa kina Kamusoko wapo wengi tu, kwahiyo nitashirikiana nao kama
nilivyoshirikiana na Haruna lakini kwaupande wangu imeniuma, ” amesema Msuva.
Msuva amesema, atamkumbuka Haruna
hususani ndani ya uwanja kwani walishirikiana kwa kiasi kikubwa
kuhakikisha wanaipa timu ubingwa misimu mitatu mfululizo.
“Haruna nitakumbuka vitu
vingikutoka kwake kwani licha ya Uwanjani pia ni mtani wangu na hata
yeye huko alipo anajua kabisa ameniacha mchezaji mwenzake sina raha
kwani tumekuwa na ushirikiano mkubwa ndani ya timu hususani katika suala
la ushauri, ni mchezaji wa kimataifa ambaye na mkubali katika soka, ” Msuva aliongeza.
No comments:
Post a Comment