Dogo Janja aruka kwa Muna Love
Msanii wa hip hop Dogo Janja
amekanusha tetesi za kujihusisha kimapenzi na muigizaji wa zamani na
mfanyabiashara Muna Love kwa kusema hajawahi kuwa na mahusiano na habari
hizo zinamuweka sehemu mbaya katika mahusiano lakini pia kifamilia.
Msanii Dogo Janja Kushoto, na Kulia ni Mfanyabiashara Muna Love
Janjaro
amelazimika kufunguka hayo baada ya tetesi kuenea muda mrefu
kujihusisha na Mwanadada huyo huku wengine wakienda mbali zaidi kwa
kusema kwamba analelewa na mfanyabiashara huyo.
"Hakuna kitu kibaya kama
utandawazi, yaani kila mtu ana simu na bando lake kwa hiyo akiamka
asubuhi anajisikia kufanya chochote au kutunga vitu kama hivyo lakini
siyo kitu kizuri, maana yananiumiza mimi na familia yangu, Uongozi wangu
lakini pia vinamuumiza mpenzi wangu kwa sababu tuna malengo makubwa
hivyo haya yanapoendelea yanazidi kumuumiza au kumchanganya", Dogo Janja alifunguka.
Aidha Janjaro ameongeza kwamba "Mimi
siyo mtu wa kuonesha maisha yangu binafsi kwenye mitandao ndio maana
hata mpenzi wangu sijawahi kumuweka mitandaoni, maisha yangu binafsi ni
ya kwangu na siyo ya kila mtu hata huyo dada wa watu anaumizwa na hili
na anafamilia pia kwa hioyo hizi habari zinazidi kumuweka pabaya.
Pamoja na hayo Dogo Janja amewataka watu
kutoamini chochote kinachoanzishwa kwenye mitandao ya kijamii mpaka
atakapozungumza mwenyewe
No comments:
Post a Comment