Marufuku kutumia madarasa kwa Wajawazito
Mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya ya
Sumbawanga, Bwana Kalolo Ntilla amepiga marufuku wanafunzi wajawazito
na waliojifungua kutumia madarasa na vituo vya shule za msingi zinazotoa
huduma ya Mpango wa Elimu ya Msingi kwa walioikosa (MEMKWA).
Mwenyekiti
huyo ametoa onyo kwa Walimu Wakuu wote wa shule za msingi kuacha mara
moja tabia ya kuwafundisha wanafunzi wajawazito au waliojifungua kutumia
vituo hivyo na kuwataka kufuata malengo ya vituo hivyo ya kutoa elimu
ya msingi kwa makundi ya watoto waliochelewa kuandikishwa na si
vinginevyo.
Mbali na hilo Bwana Kalolo amesema halmashauri yake yenye vituo kumi vya kutoa huduma ya MEMKWA katika shule za msingi 103 zilizoko kwenye halmashauri hiyo, lazima iimarishe vituo hivyo kwa lengo la kuboresha elimu.Pia ameitaka Idara ya Elimu kuanzisha vituo vingi zaidi ya vya ufundi, badala ya kimoja cha Mtowisa, ili kuwalenga waliomaliza elimu ya msingi na wale waliokatisha masomo yao.

No comments:
Post a Comment