Simba wamfunga mdomo Mnyate
Winga mwenye kasi Jamal Mnyate
aliyekosa nafasi katika kikosi cha kwanza cha Simba msimu uliopita
amefunguka na kusema kuwa bado ataendelea kuwemo katika klabu hiyo
kutokana na kuwa na mkataba na timu hiyo.
Mnyate
alisajiliwa na Simba akitokea katika klabu ya Mwadui kwa mkataba wa
miaka miwili lakini tangu alivyosajiliwa alifanikiwa kucheza mechi
kadhaa kutokana na mara nyingi akiwa anasumbuliwa na majeruhi.
Amesema hawezi kuzungumza chochote kwa
sasa kutokana na kuwa bado yupo chini ya mkataba na timu hiyo, lakini
angekuwa ameshamaliza nao mkataba angekuwa huru kusema msimu ujao
atakuwa wapi.
“Kwa hivi sasa ni ngumu
kusema msimu ujao nitakuwa wapi, kwasababu bado nina mkataba wa mwaka
mmoja na Simba kikubwa mimi nawasikiliza wao waajiri wangu
watakavyonambia kuhusu hatima yangu,”amesema.
No comments:
Post a Comment