Manula hajasaini Simba - Jaffar Iddi
Manula hajasaini Simba - Jaffar Iddi
Afisa Habari wa klabu ya
Azam, Jaffar Iddi amefunguka na kukanusha taarifa zinazoendelea mitaani
kuwa kipa namna moja wa Azam FC, Aishi Manula amesaini mkataba na klabu
ya Simba na kudai kuwa mchezaji huyo bado atabaki Azam FC.
Jaffar
Iddi amesema hayo leo wakati akiongea na waandishi wa Habari ambapo
alikuwa akitoa picha jinsi klabu ya Azam itakavyoendeshwa sasa kwa
kusema saizi wao watatoa kipaumbele zaidi kwa wachezaji wanaochipukia na
kusema klabu hiyo saizi haiwezi haiwezi kutumia gharama kubwa sana kama
ilivyokuwa kipindi cha nyuma katika usajili, huku akisisitiza kuwa
mazungumzo ya kuwabakisha Manula na Shomari Kapombe yapo katika hutua
nzuri.
"Nisema tu kwamba Aishi
Manula, Shomari Kapombe mikataba yao inakaribia kuisha lakini mazungumzo
ya Aishi Manula na Shomari Kapombe yapo katika hatua za mwisho kabisa
na nisema tu yanakwenda vizuri. Aishi Manula ataendelea kubaki Azam FC
kilichobaki saizi tunategemea wakitoka Misri basi tukamilishe taratibu
zao na ninawatoa shaka kuwa Aishi ataendelea kubaki Azam FC hata yeye
wakati anakwenda Misri na timu ya taifa aliongea na waandishi wa habari
akisema "Sitatoka Azam FC labda niende nje ya nchi nikacheze lakini kwa
timu za hapa nyumbani sitaweza kufanya hivyo" kwa hiyo kauli yake
inaenda na kauli ya klabu ni kweli alikuwa anazungumzwa kuwa anakwenda
kwenye klabu za hapa nyumbani lakini yeye mwenyewe ameweka wazi hilo" alisema Jaffar Iddi
Mbali na hilo Jaffar Iddi amesema kikosi cha Azam FC hakitakwenda
nchi yoyote ili kupiga kambi kwa ajili ya maandalizi ya msimu mwingine
wa Ligi Kuu Tanzania Bara bali wao wataweka kambi hapa hapa nchini na
kudai watakuwa Chamanzi, huku akibainisha kuwa wao wataanza maandalizi
ya msimu mpya mwezi wa saba.
No comments:
Post a Comment