Trending News>>

VIDEO : Sijiuzi - Pam Dafa

Msanii Pamela a.k.a Pam D amekanusha zile tetesi za yeye kujiuza mitandaoni na kudai yeye ni mwanamke anayejitambua na kujiheshimu hawezi kufanya hivyo.

 Msanii wa Bongo fleva Pam Dafa
 Pam D amebainisha hayo baada ya zile picha na video zake anazoonekana akikata mauno kupitia ukurasa wake wa Instagram kitendo ambacho watu wengi walimchukulia kama anajiuza na kujinadi ili kupata wanaume mtandaoni. "Sivyo ambavyo ipo, mimi ni msichana ninayejielewa, najitambua pia nipo katika mahusiano kwa muda mrefu sana kwa hiyo siwezi nikasema nina jiuza, ikiwa nina matarajio ya kuolewa kwa sababu hata kama nafanya muziki nafasi ya mwanamke itabaki kuwa ya mwanamke siku zote, muziki ni kazi kama kazi nyingine ambazo wengine wanafanya" alisema Pam D kupitia kipindi cha eNewz Mtazame hapa Pam Dafa akifunguka kwa kina zaidi.

No comments:

Powered by Blogger.