Serikali kusafirisha mwili Mzee Ngosha
Mwili wa Mzee Francis Maige
Kanyasu alimaarufu kwa jina la Mzee Ngosha ambaye anayetajwa kuwa ni
moja wa wachoraji wa nembo ya Taifa aliyefariki tarehe 30 mwezi wa 5
unatarajiwa kusafirishwa kesho kuelekea Misungwi Mwanza.
Mwili wa Mzee Francis Maige Kanyasu alimaarufu kwa jina la Mzee Ngosha enzi za uhai wake, akiwa anapatiwa matibabu katika Hospitali ya Muhimbili.
Kwa
mujibu wa taarifa ya Katibu Mkuu Wizara ya Afya (Maendeleo ya Jamii)
imesema kuwa ndugu wa Mzee Kanyasu wamepatikana na sasa serikali
itagharamia kusafirisha mwili wa mzee huyo mpaka Mwanza ambapo atakwenda
kuzikwa huko.
Mwili wa Mzee Francis Maige unatarajiwa kuagwa kesho Jumamosi saa 2 asubuhi Hospitali Taifa ya Muhimbili kabla ya kuanza safari ya kuelekea Mwanza.
Mwili wa Mzee Francis Maige unatarajiwa kuagwa kesho Jumamosi saa 2 asubuhi Hospitali Taifa ya Muhimbili kabla ya kuanza safari ya kuelekea Mwanza.
No comments:
Post a Comment