Maisha magumu ya chumba kimoja ya Cristiano Ronaldo na dada zake enzi hizo
Jina lake kamili ni Cristiano Ronaldo dos Santos Aveiro alizaliwa February 5, 1985 Funchal, Madeira kisiwa kidogo kilichopo pwani ya Magharibi Ureno, Ronaldo ni mtoto wa nne katika watoto wanne waliyozaliwa katika familia ya Maria Dolores dos Santos na Jose Dinis Aveiro.
Jina la Ronaldo lilitokana na baba yake kumpenda sana aliyekuwa Rais wa 40 wa Marekani Ronald Reagan, maisha ya utoto ya Cristiano Ronaldo yalikuwa na changamoto nyingi na maisha magumu, baba yake Jose Dinis Aveiro kazi yake ilikuwa ni kutunza bustani na alifariki mwaka 2005 kwa matatizo ya figo yalitokana na ulevi wa kupindukia.
Ronaldo akiwa na baba na mama yake
Ronaldo akiwa na kaka yake Hugo Aveiro na dada zake Katia Aveiro na Elma Aveiro
Mwaka 2002/3 akafanikiwa kuichezea Sporting CP timu B na baadae akaingia timu ya wakubwa, kingine ambacho hufahamu Cristiano Ronaldo akiwa na umri wa miaka 15 aliwahi kufanyiwa upasuaji baada ya kugundulika kuwa na tatizo la racing heart.
Cristiano Ronaldo alikuwa maarufu shuleni kwa wanafunzi wenzake na alifukuzwa shule baada ya kumtupia kiti mwalimu, Ronaldo hadi leo huwa anakiri kufanya kosa hilo lakini anaamini mwalimu alimkosea heshima ndio maana alifanya hivyo kwa hasira.
Baada ya kufukuzwa mama yake Maria akamwambia hakuna namna ni kuongeza bidii katika soka pekee ndio kunaweza kumkomboa katika maisha, ugumu wa maisha uliwahi kumfanya mama Ronaldo ahisi kuwa mwanae anaweza kuingia katika matumizi ya madawa.
Alipojiunga na Andorlinha
“Nilipokuwa mdogo niliwahi kumwambia baba yangu kuwa sisi tutakuwa matajiri na tutakuwa na nyumba kubwa, aliniambia hiyo haiwezekani, leo hii ninachokile nilichoahidi kwa baba yangu lakini ndio sipo nae tena” >>>> Cristiano Ronaldo
No comments:
Post a Comment