Trending News>>

Simba imeingia mkataba na mchezaji wa sita leo


Wekundu wa Msimbazi Simba bado wanaonesha kudhamiria kufanya vizuri katika mashindano mbalimbali msimu ujao, dhamira hiyo imeoneshwa kwa kuendelea na jitihada zao za kuingia mikataba na wachezaji mbalimbali mahiri.
Baada ya jana kumtangaza rasmi John Bocco aliyekuwa Azam FC kujiunga nao, leo June 14 2017 imetangaza kuingia mkataba wa miaka miwili na aliyekuwa golikipa wa Mbao FC Emmanuel Elias Mseja.
Kama utakuwa unakumbuka vizuri golikipa Emmanuel Mseja anakuwa mchezaji wa sita kuungana na Simba baada ya Yusuph Suleiman, Jamal Mwambeleko, Shomari Kapombe, Aishi Manula na John Raphael Bocco.

No comments:

Powered by Blogger.