Wenger bado yupo yupo sana Arsenal
Kocha wa Arsenal Arsene
Wenger amekubali mkataba mpya wa miaka miwili, unaomuongezea utawala wa
miaka 21, kwenye klabu hiyo ya Emirates.
Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger
Wenger
alikutana na mmiliki wa klabu Stan Kroenke Jumatatu kutathmini
mustakabali ujao wa Mfaransa huyo, na maamuzi zaidi yalirudishwa kwenye
bodi ya wakurugenzi ya klabu.
Arsenal wanapanga kutoa taarifa maalum
Jumatano, kumsimika tena Mfaransa huyo, aliyeweka rekodi mpya ya
kushindwa kufuzu michuano ya ligi ya mabingwa Barani Ulaya, kwa mara ya
kwanza baada ya miaka 21, tangu Arsenal imalize nafasi ya tano msimu
uliomalizika.
Washika mitutu hao wa Emirates,
walimaliza wakiwa pungufu ya pointi 18 nyuma ya mabingwa Chelsea, lakini
waliifunga the Blues 2-1 kwenye fainali ya FA uwanja wa Wembley
Jumamosi iliyopita.
Mkataba wa Wenger ulikuwa unamalizika
mwishoni mwa msimu huu, na ungehitimisha miaka 21 ya kocha huyo tangu
ajiunge na timu hiyo, mwaka 1996.
Matukio ya kukumbukwa kwa Wenger;
Aliiongoza the Gunners kutwaa mataji
matatu ya ligi kuu ya soka nchini Uingereza na makombe manne ya chama
cha soka FA katika kipindi chake cha kwanza cha miaka 9.
Mnamo mwaka 2003-04, alikuja kuwa kocha
wa kwanza tangu 1888-89 kuingia kwenye rekodi ya kutwaa ubingwa wa EPL
bila ya kupoteza mechi.
No comments:
Post a Comment