Magufuli ataigwa duniani kote - Serukamba
Mbunge wa Kigoma Kaskazini
(CCM), Peter Serukamba amefunguka na kusema jambo alilofanya Rais
Magufuli kuzuia mchanga litakwenda kuigwa duniani kote na kuleta
mapinduzi katika "Extractive Industries" (sekta za uchimbaji madini)
Serukamba
alisema hayo jana bungeni na kusema ukiona mpinzani wako anakupinga
katika jambo lolote lile basi ujue umefanya jambo ambalo ni sahihi ila
ukiona mpinzani wako anakusifu ujue umefanya jambo baya, hivyo kwa kuwa
wapinzani wanalalamika basi Rais amepatia katika maamuzi yake, na
anatakiwa kupewa ushirikiano wa wananchi na wabunge.
"Mimi kama mwanasiasa ukiona
mtu ambaye ni adui yako umefanya jambo akakusifia ujue lipo tatizo, ila
ukiona umefanya jambo adui yako akasema umekosea maana yake umepatia
sana. Mimi naomba nimpongeze Rais Magufuli kwa kazi kubwa aliyofanya na
niwaambie waheshimiwa wabunge, duniani kote 'Extractive Industries'
inaenda kubadilika atakaye kuwa kwenye historia ya kubadilisha
Extractive Industries ni Rais Magufuli, leo duniani kote kila kwenye
migodi mambo yatabadilika kwa sababu ya Magufuli amefungua milango,
niwaambieni watanzania tusiogope kwenye hili lazima tuwe nyuma ya Rais
tumuunge mkono aendelee na nina hakika wawekezaji watakuja mezani" alisisitiza Serukamba
No comments:
Post a Comment