WATATU WALIOSHITAKIWA KWA KESI YA MADAWA YA KULEVYA WAACHIWA HURU
Na Karama Kenyunko, Blogu ya jamii.
Mahakama
ya Hakimu Mkazi Kisutu imewafutia kesi washtakiwa watatu waliokuwa
wanakabiliwa na kesi ya dawa za kulevya zenye thamani ya zaidi ya
milioni 25 na kuamuru wasikamatwe.
Amesema
washtakiwa hao wasikamatwe na kushtakiwa kwa kufunguliwa shtaka
linalofanana na hilo labda kwa maelekezo ya Mahakama Kuu.
Hatua
hiyo ua kufuta kesi hiyo imekuja baada ya washtakiwa kuwa rumande kwa
zaidi ya miaka mitatu bila ya upelelezi kukamilika na jalada ya polisi
kutokuwepo mahakamani mara kadhaa. Washtakiwa walioachiwa huru ni, Salma
Juma , Amos Sosoma na Rashid Mtitu.
Kesi
hiyo iliyokuwa na namba 21 ya mwaka jana imefutwa na Hakimu Mkazi Mkuu,
Respicius Mwijage baada ya kukaa mahakamani hapo kwa miaka mine bila ya
upelelezi kukamilika.
Amesema
Machi 6, mwaka huu, mahakama iliamuru upande wa mashtaka ifikapo Machi
23, itoe taarifa juu ya hatua ya upelelezi lakini ilipofika siku hiyo
upande wa mashtaka ulidai upelelezi bado haujakamilika na jalada la
polisi halipo.
Akiendelea
kusoma uamuzi huo Hakimu Mwijage alisema kesi iiahirishwa hadi Aprili
5, mwaka huu lakini upande wa mashtaka ulibaki na jibu lile lile kuwa
upelelezi haujakamilika na kuomba wapangiwe tarehe nyingine.
Hata
hivyo baada ya kauli hizo kuebndelea kutawala mahakamani hapo mara
kadhaa, washtakiwa walilalamika kuwa walifikishwa mahakamani Agosti 26,
2013.Walidai kuwa, kesi yao ilipita katika mahakama mbalimbali mbapo
Juni 14, 2016 waliachiwa huru lakini walikamatwa tena na kupandishwa
mahakamani hapo na kuendelea kusota rumande.
Katika
kesi hiyo ambayo waliachiwa huru kabla ya kukamatwa tena walikuwa
wakidaiwa kukutwa na dawa za kulevya aina ya bangi kilo 920, zenye
thamani ya milioni 138.
Katika
uamuzi wake, Hakimu Mwijage amesema upande wa mashtaka Juni 14, 2016
uliwafungulia kesi nyingine mbele yake wakidaiwa kukutwa na gramu
169,500 za dawa za kulevya aina ya Bangi zenye thamani ya Sh 25,
425,000.
Hakimu
Mwijage alisema tangu Juni 14, mwaka jana hadi Aprili 5,mwaka huu,
upelelezi haujakamilika na wala Upande wa mashtaka hawana jalada la
[polisi.
“Tunawezaje
kupiga vita dawa za kulevya kama upelelezi hauwezi kukamilika kwa zaidi
ya miaka mitatu, magerezani kuna mrundikano wa mahabusu na kuna kesi za
Meno ya Tembo na dawa za kulevya ambazo upelelezi wake unacheleweshwa
bila ya kuwepo sababu za msingi.”Amesema Mwijage.
Ameongeza
mahakama ipo kwa ajili ya kutenda lakini wanachokifanya upande wa
mashtaka siyo kuendesha kesi bali ni kuwanyanyasa washtakiwa.“Kwa maoni
yangu kesi ya jinai siyo ya kuchezea, shauri hili lilipaswa kusikilizwa
Mahakama Kuu kutokana na hoja na malalamiko ya washtakiwa, mahakama hii
inayo mamlaka ya kuchukua hatua na kutoa maamuzi.” Amesema Hakimu
Mwijage.
Alibainisha
kuwa anafahamu kwa mujibu wa sheria hakuna muda wa upelelezi wa kesi
kama ya aina hiyo, ila amezingatia mazingira ya kesi , malalamiko ya
washtakiwa, na taarifa upelelezi haujakamilika kwa siku 1335.
Amesema
kitendo cha kucheleweshwa kukamilika kwa upelelezi dhidi ya kesi hiyo
imeonesha hakuna ushahidi dhidi ya washtakiwa kwa nia ya kutenda haki na
kuepuka kwenda kinyume na sheria mahakama imeifuta kesi hiyo na kuamuru
washtakiwa hao wasikamatwe na kushtakiwa kwa kufunguliwa shtaka
linalofanana na hilo labda kwa maelekezo ya Mahakama Kuu.
No comments:
Post a Comment