BALOZI SEIF ALI IDD AONGOZA MAZISHI YA MAMA MZAZI WA VUAI ALI VUAI.
NA IS-HAKA OMAR, ZANZIBAR.
MAMIA
ya Wananchi wameudhuria mazishi ya Mama mzazi wa Naibu Katibu Mkuu
mstaafu wa CCM Zanzibar.Vuai Ali Vuai, Marehemu Bi.Mwanaisha Hassan Vuai
huko Kijijini kwao Bwejuu, Mkoa wa Kusini Unguja.
Mazishi
hayo yameongozwa na Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali
Idd, aliyeambatana na viongozi mbali mbali wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)
na serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar pamoja na jamhuri ya muungano
Tanzania.
Bi. Mwanaisha amefariki jana wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Tasakhtaa iliyopo Vuga Mjini Zanzibar.
Akizungumza
mara baada ya mazishi hayo, Naibu Katibu Mkuu mstaafu wa CCM Zanzibar,
Nd. Vuai Ali Vuai alisema kifo cha Mama yake mzazi kimeacha pengo kubwa
katika familia hiyo kwani marehemu huyo alikuwa akitegemewa na jamii
kutokana na busara zake.
Aidha
Vuai amewashukru wananchi mbali mbali waliojitokeza kumuunga mkono
katika mazishi hayo na kuwasihi waendelee kuwa na umoja wa kushirikiana
katika mambo mbali mbali ya kijamii.
“
Mama yetu tulimpenda sana lakini ndio hivcyo amefariki sasa kilichobaki
kwetu sisi tuliobaki ni kumuombea dua yeye pamoja na wazee wetu wengine
waliofariki kabla yake.”, alisema Naibu Katibu Mkuu huyo.
Mbali
na Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd pia Mazishi
hayo yameudhuriwa na Viongozi mbali mbali wakiwemo Katibu Mkuu wa CCM
Abdulrahman Omar Kinana, Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dkt.
Abdalla Juma Saadala “ Mabodi”,Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Tanzania Shaka
Hamdu Shaka, Mkuu wa Mkoa kusini Unguja Dk.Idrissa Muslim Hija,
Katibu wa Kamati Maalum ya NEC, Idara ya Itikadi na Uenezi Zanzibar,
Waride Bakari Jabu.
Viongozi
wengine ni Mkuu wa Wilaya ya Kusini Unguja, Idrissa Kitwana Mustafa,
Mnadhimu wa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wa CCM, Ali Salum Haji
pamoja na baadhi ya Mawaziri, Manaibu Mawaziri na Makatibu wakuu wa
serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Bi.Mwanaisha Hassan Vuai amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 85 ameacha watoto tisa (9) pamoja na wajukuu kadhaa.
Mungu ailaze roho ya marehemu pahali pema peponi-Amin.
Makamo
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balosi Seif Ali Idd akipokelewa na
viongozi mbali mbali wa Chama na Serikali mara baada ya kuwasili katika
mazishi ya Mama mzazi wa Naibu Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM Zanzibar Vuai
Ali Vuai, huko kijijini kwao Bwejuu.
Viongozi
mbali mbali wa Chama na serikali pamoja na wananchi wakiiombea Dua
Maiti ya Bi. Mwanaisha Hassan Vuai ambaye ni Mama mzazi wa Naibu Katibu
Mkuu Msitaafu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai katika msikiti wa kijiji
cha Bwejuu.
Viongozi
mbali mbali wa Chama na serikali pamoja na wananchi wakiiombea wakiwa
msikitini kabla ya kuanza kuiswalia Maiti ya Bi. Mwanaisha Hassan.
Baadhi
ya Viongozi na wananchi kwa upande wa wanawake wakiomba dua katika
mazishi ya Marehemu Bi. Mwanaisha Hassan Vuai ambaye ni Mama mzazi wa
Naibu Katibu Mkuu Msitaafu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai katika msikiti
wa kijiji cha Bwejuu.
Matukio tofauti ya kubebwa kwa maiti inapotolewa msikiti hadi sehemu ya kaburi ilipofanyiwa mazishi.
Viongozi
mbali mbali wa Chama na serikali wakiongozwa na Katibu Mkuu wa CCM, Nd.
Abdulrahman Omar Kinana wakimfariji Naibu Katibu Mkuu mstaafu wa CCM
Zanzibar katika mazishi ya Mama yake mzazi yaliyofanyika huko kijijini
kwao Bwejuu, Mkoa wa Kusini Unguja.( PICHA NA AFISI KUU CCM ZANZIBAR).
No comments:
Post a Comment