DKT. NCHIMBI AAGIZA HALMASHAURI KUANZISHA BENKI ZA WANA MICHEZI NA KUTENGA VIWANJA VVYA MICHEZO MKOANI SINGIDA.
Halmashauri
zote saba za Mkoa wa Singida zimeagizwa kutenga maeneo yenye hadhi ya
kuwa viwanja vya michezo pamoja na kuhakikisha zinakuwa na benki ya
wanamichezo katika halmashauri zao.
Mkuu
wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi ametoa maagizo hayo leo asubuhi
kabla ya kuzindua mashindano ya michezo kwa shule za Sekondari
(UMISSETA) kwa ngazi ya mkoa ambapo wanamichezo hao wataunda timu za
Mkoa kwa ajili ya mashindano ya kitaifa yatakayofanyika jijini Mwanza
mwezi ujao.
Dkt.
Nchimbi amesema halmashauri zimekuwa zikiwatelekeza wanamichezo mahiri
hivyo wakianzisha benki ya wanamichezo kwa maana ya kuhifadhi kumbukumbu
za wana michezo mahiri pamoja na kuwaendeleza hawatapata shida kipindi
cha mashindano yoyote.
Ameongeza
kuwa halmashauri zimekuwa zikijisahau katika kuandaa maeneno ya michezo
hadi inapofika kipindi cha UMISETA hali inayopelekea kukosekana kwa
viwanja vya kufanyia mazoezi ili kuwa na timu bora.
Dkt.
Nchimbi amewaasa wana michezo kuwa na nidhamu, utii, bidii na kuitumia
michezo kuutangaza Mkoa wa Singida wenye fursa nyingi za uwekezaji
pamoja na kujitangaza uwezo wao ili waweze kupata nafasi katika timu
mbalimbali za kitaifa.
Aidha
amewasisitiza waamuzi wa michezo kutenda haki kwakuwa matendo yao ni
darasa la nidhamu na maadili kwa wanafunzi wao na kuwatahadharisha
wanafunzi wasio tii kuwa hawatapata nafasi katika timu ya Mkoa.
Kwa
upande wake Katibu Tawala Mkoa wa Singida Dkt Angelina Mageni Lutambi
amewapongeza wakurugenzi wa halmashauri kwa kufanikisha upatikanaji na
ushiriki wa timu za michezo za kila halmashauri.
Dkt.
Lutambi ameishukuru pia kampuni ya Coca cola kwa udhamini wa UMISSETA
kwa kutoa vifaa kwa shule 118 ambavyo ni tisheti 3,776, mipira ya miguu
118 na mipira ya basketball 118 pamoja na ahadi ya kuendelea kugawa
vifaa katika shule 45 zilizobaki.
Ameongeza
kwa kuwasihi wana michezo wote kucheza kwa nidhamu ya hali ya juu, kwa
kuzingatia sheria na kanuni za michezo ili kutengeneza timu ya ushindi
ya mkoa.
Akisoma
taarifa ya Michezo ya Umiseta Afisa Michezo wa Mkoa Henry Kapella
amesema jumla ya wana michezo 576 wameshiriki katika michezo hiyo ambapo
wataunda timu ya mkoa ya michezo ya bao, riadha, mpira wa miguu na
mpira wa pete.
Kapella
ameongeza kuwa kauli mbiu ya michezo ya Umisseta kwa mwaka 2017 ni
‘Wekeza katika michezo kwa ustawi wa elimu na Viwanda’.
Kwa
upande wao wanafunzi walioshiriki mashindano ya umisseta wamesema
michezo inawajenga kiafya na kiakili kwa kuwa wanafunzi wanaoshiriki
katika michezo huwa na ufaulu mzuri wa masomo yao.
Wameongeza
kuwa michezo inawaongezea nidhamu na kuwajenga kimaadili hivyo kufaulu
inakuwa ni rahisi, aidha wamesema michezo ina faida nyingi ikiwemo
kuwatengenezea ajira mara baada ya kumaliza masomo yao.
Mkuu
wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi (aliyenyanua ubao) akipiga ubao
wa kuashiria uzinduzi wa michezo ya UMISSETA mkoa wa Singida, mbele yake
ni wanariadha wakianza mashindano.
Wanamichezo
kutoka Shule za Sekondari za Halmashauri ya wilaya ya Itigi wakiimba
wimbo wa taifa kabla ya kuanza mashindano ya UMISSETA ngazi ya Mkoa.
Mkuu
wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi (katikati) akiimba wimbo wa
taifa kabla ya kuanza mashindano ya UMISSETA ngazi ya Mkoa, kushoto
kwake ni Katibu Tawala Mkoa wa Singida Dkt. Angelina Mageni Lutambi na
Kulia Kwake ni Afisa Elimu Mkoa wa Singida Florian Kimolo.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akihutubia kabla ya kuzindua mashindano ya UMISSETA ngazi ya Mkoa wa Singida.
Katibu
Tawala Mkoa wa Singida Dkt. Angelina Mageni Lutambi akizungumza katika
uzinduzi wa mashindano ya UMISSETA Mkoa wa Singida.
Afisa
Michezo wa Mkoa wa Singida Henry Kapella akisoma taarifa ya michezo ya
Umisseta wakati wa uzinduzi wa mashindano hayo ngazi ya Mkoa.
No comments:
Post a Comment