SIMULIZI :: Jini Mahabati Sehemu ya Kumi na Tatu (Kwa wenye miaka 18+)
SIMULIZI : JINI MAHABATI
SEHEMU YA KUMI NA TATU
MTUNZI:MANYAMAJR
AGE: 18+
ILIPOISHIA
Kila mmoja aliingiwa na huzuni wasijue nini kilitokea,Radhia siku hiyo alikwa na hofu sana hivyo alimwomba rafiki yake Halima walale wote. Ingawa Halima naye alikuwa na woga sana lakini alijikaza na kulala na rafiki yake huyo.Usiku Radhia alijiwa na ndoto ya maelekezo ya nini anatakiwa kukifanya. Mzimu wa Barike ulimtokea na kumweleza kuwa kwa nini wamemdhuru Tariq. “Tariq ni kijana anayekupenda sana lakini tatizo lake moja ni kwamba anataka kujaribu kutufautilia fuatilia hivyo tunakuomba ukae mbali naye kama na wewe unataka kweli uishi kwa amani na furaha hapa duniani ilikuwa ni baadhi ya mazungumzo ya ana kwa ana ya Radhia na jini Barike kupitia ndoto.***
TIRIRIKA NAYO.
Ndoto hiyo ya maelekezo juu ya nini kifanyike na kumsihi Radhia akae mbali sana na kijana huyo ilimfanya binti huyo ashituke kutoka usingizni.Akajikuta mwili mzima umejaa jasho na mashuka yamelowa.Mapigo ya moyo ya binti huyo yakaongezeka hofu na woga usiku huo pia vikamtawala. Akaangalia pembeni akakuta ndo kwanza rafiki yake Halima anakoroma na kuweweseka kwa ishara kuwa na yeye alikuwa akiota ndoto nzuri.Radhia kwa woga ilibidi amtingishe tingishe rafiki yake huyo.Halima akajigeuza mara mbili kisha akageukia upande wapili na kuendelea kupiga usingizi.Ilibidi Radhia amuache tu maana alihisi kuwa rafiki yake huyo na yeye labda alikuw aakioteshwa vitu vingine.Radhi hakuwa na hamu tena ya kulala zaidi aliamua kuamka na kuchukua lap top yake na kuanza kufanya lile swali lililomleta Halima hapo.Akawasha lap top yake mara ya kwanza ikawaka na kuzima.Bado akajipa moyo akaamua kuwasha kwa mara ya pili lakini pia ilirudia mcheo ule ule.. “Aaaaaah,, ahaaaaaaaaaaaaaaa Radhia binti uliye ridhiwa huu ni mda wako wa kupumzika tunaomba uwe mtiifu ulale”ilisikika sauti ya kike ambayo Radhia alikuwa ameshaizoea na si nyingine bali ilikuwa ya jini Barike au maarufu kama jinni mahabati.
Radhia akazidi kuchachawa hofu na huzuni vikazidi kutawala. Akarudi kitandani akajilaza na kwa uwoga alichukua shuka lake na kujifunika gubigubi. Ile sauti ikasikikia ikisema “ukiendelea na utiifu huo basi ni lazima utafanikiwa na sisi tutakusaidia kufanya shughuli zako zingine uwe na usiku mwema binti uliyedhiwa.” Radhia akafunga macho na kuutafuta usingizi ambao ulikuja kiulaini siku hiyo tofauti na siku zingie. Si Radhia si Halima wote walilala kama magogo na walikuja kushituka ilikuwa ni asubuhi pamepambazuka na siku hiyo kulikuwa na vipindi vya asubuhi.
Wakaamka wakajiandaa tayari kwa kwenda chuoni. Kabla hawajaondoka Radhia aliamua kuwasha laptop yake mbele ya Halima ili aweze kuona je yale maluwiluwi yaliyomtokea usiku siku yatatokea tena au la.
Safari hii laptop iliwaka vizuri lakini pia kuna kitu cha ajabu alikutana nacho. Kwanza ile picha ya Tariq aliyoiweka kama background ya laptop hiyo haikuonekana na badala yake ilionekana picha kama hiyo inayonekana kwenye background ya profile picha ya kitabu hiki. Yaani kulionekana binti mrembo sana lakini kwa upande wa kichwani alikuwa na kama vipembe viwili na chini kama kimkia kifupi.
Kwa kifupi ni kama zile picha za kubuni za majni. Radhia aliangalia ile picha na kujikuta akiingwa na uwoga tena asubuhi hiyo. Radhia akamuuliza rafiki yake ambaye alikuwa bado anajiremba remba huku akichagua nguo za Radhia ili aweze kuvaa siku hiyo kuwa lile swali walilotaka kulifanya alilisevuje. Nililisevu kama Sociology question alijibu Halima. Hapo ikampa nafasi Radhia kulitafuta swali hilo.
Akaenda sehemu ya kusearch na kuandika kama alivyotajiwa. Cha ajabu badala ya kuja swali kama swali ilikuja assignment ambayo ilikwishafanywa. Jamani wewe Halima kwani ulishafanya hili swali ilibidi Radhia aulize huku akitirika kusoma assignment hiyo ambayo ilikwisha fanywa na ilifanywa kwa ufundi mkubwa sana. “Hapana shosti ningelifanya saa ngapi wakati jana nimekukuta ukiwa ulimwengu mweingine wa raha za dunia alijibu Halima.
Radhiai akasoma mpaka mwisho na alipomaliza akajisemaa kweli hivi viumbe vya jabu vimeniridhia na kweli vinanisaidia.
Hali ya afya ya Tariq ikazidi kuwa mbaya sana na haikujulikana alikuwa akiumwa ugonjwa gani. Afya ikazidi kuzoofu siku hadi siku hivyo ikabidi aombe ruhusa na kurudi nyumbani. Hali hiyo pia ilimsistua sana Radhia na akazidi kuwa njia panda asijue nini kinaendelea. Tariq alirudi kwao ambapo baba yake alizidi kumwangaikia mwanaye huyo bila mafanikio. Baba yake pia alikuwa na elimu juu ya viumbe hivyo vya majini. Elimu hiyo ndo alikuwa akiitumia mwanaye kusema kuwa anahisi Radhia alikuwa anaongozwa na jinni.
Lakini pamoja na elimu hiyo bado walikuwa wakipata tabu sana kumpa tiba Tariq na hawakujua ni nini kilimkumba japo kulikuwa na uelewa wa moja kwa moja kuwa alipata madhara mara baada ya kujaribu kufuatilia habari za Radhia.
Kwa upande wa Radhia yeye aliendelea na maisha ya chuo mpaka ukafika mda wa mitihani. Na kipindi hicho lile jinni mahabati lilikuwa limepunguza kasi na kumwacha Radhia aweze kufanya mitihani yake kwa urahisi. Wanafunzi wa darasani kwao waliumia sana kuona kijana Tariq kipenzi cha wengi ameshindwa kufanya mitihani hiyo ya kumalizia semista. Kulikuwa hakuna jinsi maana ndo ishatokea tu itabidi kijana huyo airishe masomo au atafute mbinu zingine za kuendelea na masomo. Mitihani ilikwisha na sasa ilikuwa ni kipindi cha likizo ambapo Radhia alikuwa akirudi jijini Dar es Salaam sehemu ambapo wazazi wake walikuwepo.
Lakini kabla ya kwenda Dar alipata wazo kuwa apitie pangani Tanga sehemu ambayo kina Tariq walikuwa wakiishi.
Radhia alifikiria sana hadhma yake hiyo ya kwenda kumuoana rafiki yake huyo lakini bado alikuwa dilema maana hakujua kama itamletea madhara au la. Alitamani kama angekuwa na uwezo wa kuongea na wale viumbe angewauliza kama ni sahihi kwa yeye kwenda kuwasalimia au la.
Baadaye akaamua kufanya maamuzi yeye mwenyewe kuwa ngoja aende tu alafu lolote litakalotokea huko atapambana nalo. Usiku wa siku hiyo jinni Barike lilimjia ndotoni na kumuonya kuwa hasijaribu kabisa kufanya hicho alichokuwa akitaka kukifanya maana kitamletea madhara makubwa sana. Ndoto hiyo ikazidi kumweka dilemma binti huyo hasijue atafanya nini kumsaidia Tariq maana alihisi kabisa kijana huyo atakuwa kwenye matatizo makubwa sana.
Ujue licha ya kwamba Radhia hakuawahi kufanya mapenzi na Tariq lakini ukweli ni kamba alikuwa akimpenda sana kijana huyo tena upendo wa dhati upendo kutoka moyoni.
Radhia usiku wa siku hiyo alishangaa tena ule muwasho ambao ulitulia takribani kwa mda wa mwezi mmoja ukimuanza kumsumbua. Kile kitu ambacho kilikuwa kikimtekenya tekenya na kumsumbua kikamuanza tena. Alitamani kuamka usiku huo huo kwenda kutafuta mtu wa kumkuna. Lakini tatizo ilikuwa ni usiku sana na hakujua nini cha kufanya. Akawaza kurudia ile tiba yake ya kujikanda kanda na maji ya moto lakini akaona bado haitomsadia kitu maana ni sawa tu na kujizalilisha.
Akachukua simu yake kisha akaanza kupitia namba moja baada ya ingine nia ni kutafuta namba ya mtu yeyote ambaye yupo karibu anaweza kumpigia na kumwambia kuwa anashida. Radhia usiku huo alikuwa ni kama mtu aliyechaganyikiwa maana hakujua hata kama huo ulikuwa ni usiku wa manane. Akaanza kukutana na namba ya baba Juma baba mwenye nyumba.
Akaanza kuipiga lakini akili zikamrudi haraka haraka akakata na maana alijua inaweza kuleta majanga kwa kuwa mama Juma alikuwepo siku hiyo. Akaendelea kutafuta namba zingine kama zilivyopanga kialufabeti katika simu yake.
****ITAENDELEA*****
No comments:
Post a Comment