Polisi afyatua Risasi Hewani baada ya kutibuana na Adam Malima
TAHARUKI imeibuka mchana wa leo maeneo ya Masaki karibu na
Double Tree Hotel baada ya askari polisi mmoja kufyatua risasi hewani
kutokana na kile kilichoonekana kuwepo kwa mzozo kati ya polisi na
mbunge wa zamani wa Mkuranga, Pwani, Adam Kighoma Ali Malima.
Taarifa zimeeleza kuwa chanzo cha tukio hilo yalikuwa ni majibizano kati ya Majembe Auction Mart waliokuwa wameambatana na polisi walipojaribu kukamata gari lililokuwa limeegeshwa barabarani.
Inasemekana gari lilikuwa la mwanaye Kighoma Malima aliyekuwa eneo hilo kwa shughuli zake binafsi ambapo ofisa wa Majembe alivamia gari hilo na alipodaiwa kuonyesha vitambulisho aligoma kutoa ndipo wananchi walipolizingira gari wakitaka kumpiga wakizania ni jambazi.
Polisi aliingilia kati na katika majibizano ya maneno na Malima, ndipo askari mmoja akafyatua risasi kadhaa hewani hali iliyozua taharuki kubwa eneo hilo.

No comments:
Post a Comment