Miaka saba jela kwa kuiba kichanga
Mahakama ya Wilaya ya Mbozi mkoani Songwe imemhukumu kifungo cha miaka
saba, Happness Mwakisyala (28) mkazi wa Majengo, Tunduma baada ya
kukiri kosa la kutaka kumuiba mtoto mchanga wa umri wa saa 12 kwenye
hospitali ya wilaya hiyo.
Hakimu wa Mahakama hiyo, Nemes Chami amesema baada ya mshtakiwa huyo kukiri mwenyewe kosa hilo, mahakama ilijidhirisha maelezo yake hivyo kumhukumu kifungo cha miaka saba gerezani ili iwe fundisho kwa wengine kwani vitendo hivyo vimeanza kushamiri katika jamii wilayani hapo.
“Mahakama haioni sababu ya kuchukua muda mrefu katika shauri hili, kwa sababu mshtakiwa mwenyewe amekiri kosa lake, na mahakama imejiridhisha maelezo yake na yaliyotolewa upande wa Jamhuri, hivyo inamtia hatiani mshtakiwa huyo na atakwenda jela miaka saba,”amesema.
Awali mwendesha mashtaka, Samwel Siro aliiomba mahakama kutoa adhabu kali kwa mshtakiwa kutokana na vitendo vya kuiba watoto kukithiri hivi sasa katika jamii ili iwe fundisho kwa wengine wenye nia kama hiyo.
Mshtakiwa huyo alidaiwa kutenda kosa hilo saa 11 alfajiri ya Mei 11, mwaka huu ambapo kwa makusudi aliingia kwenye wodi ya wazazi katika hospitali ya Wilaya ya Mbozi na kumuiba mtoto wa kiume kisha kwenda kumficha chooni kabla ya kuondoka naye.

No comments:
Post a Comment