Mapambano dhidi ya wahamiaji haramu Rukwa
WIMBI la wahamiaji haramu kutoka nchi jirani ya DRC limedaiwa
kuwa kikwazo cha utoaji wa huduma kama chanjo, magonjwa ya mlipuko na
vita dhidi ya ugonjwa wa Ukimwi katika mwambao wa Ziwa Tanganyika katika
wilaya za Nkasi na Kalambo mkoani Rukwa na kuwalazimu madiwani wa
wilaya ya Nkasi kuiomba Serikali kushughulikia haraka suala hilo.
Baraza la madiwani la Halmashauri ya wilaya ya Nkasi limeezwa kuwa katika kata za mwambao wa Ziwa Tanganyika kumekuwa na wimbi kubwa la wahamiaji haramu wengi wao wakitokea nchi jirani ya DRC.
Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Nkasi na mkuu wa wilaya amekiri kuwepo kwa wahamiaji haramu katika wilaya yake.

No comments:
Post a Comment