Trending News>>

Meya Édouard Philippe achaguliwa kuwa waziri mkuu Ufaransa

Rais mpya wa Ufaransa, Emmnauel Macron, amemchagua aliyekuwa Meya wa mji wa Kasakazini wa Le Havre Édouard Philippe, kuwa waziri mkuu mpya.

Uteuzi huo unadaiwa kuwa mpango wa rais Macron kuzivutia pande zote za kisiasa za mrengo wa kushoto na kulia nchini Ufaransa.

Bw Philippe, mwenye umri wa miaka 46, ambaye alipigiwa upatu na wengi, sio mwanachama wa Chama cha rais Macron cha République en Marche.

Tangazo hilo limetajwa kuwa muhimu kwa Rais Macron anayalenga kufanya vyema katika uchaguzi wa ubunge.

Rais Macron anasaka uungwaji mkono wa kutekeleza mipango yake ya kufanya marekebisho ya kiuchumi.

Hatua hiyo ni ya kwanza ya rais Macron baada ya kuanza kazi rasmi leo siku moja tu baada ya ya kuapishwa kabla ya uchaguzi wa ubunge mwezi ujao.

Baadaye Bw Macron atasafiri hadi Ujerumani kukutana na kiongozi wa taifa hilo, Chansela Angela Merkel.

Wawili hao wanatarajiwa kujadili masuala ya kiuchumi ya bara Ulaya ikiwemo kutenga bajeti maalum na kuwa na waziri wa fedha wa bara Ulaya.

Kiongozi huyo aliye na miaka 39, ambaye ni waziri wa zamani wa Uchumi, alikabidhiwa mamlaka siku ya jumapili na Francois Hollande katika kasri ya Élysée

Ameahidi kuwaridhisha raia wake kuwa nguvu za Ufaransa hazijadidimia na kuwa nchi hiyo iko katika hali ya mabadiliko makubwa.

Wadhfa huo hauna nguvu zaidi huku baadhi ya majukumu yakiwa ni kufanikisha mipango ya Rais na kumwakilisha katika baadhi ya mikutano.

Chama cha rais Macron cha République en Marche ina zaidi ya wawaniaji 400 watakaoshiriki uchaguzi wa mwezi Juni.

No comments:

Powered by Blogger.