Trending News>>

INASIKITISHA SANA: NI VILIO KWA MARA NYINGINE MIILI YA WANAFUNZI WALIOZAMA ZIWA VICTORIA YAPATIKANA



Nimeipata hii taarifa kutoka mkoani Geita ikieleza kumetokea ajali ya Mtumbwi ambao ulibeba wanafunzi wa shule ya Ludegea ambapo wanafunzi watatu wamepoteza maisha baada ya kuzama na wengine 21 wamenusurika.
Imeelezwa kuwa wanafunzi hao walikuwa njiani kuelekea shuleni wakati ajali ya kuzama mtumbwi huo ilipotokea.  Wanafunzi watatu kati ya 24 wa shule ya msingi Butwa, waliozama katika ziwa Victoria, kisiwa cha Butwa, wamefariki dunia.
Awali wanafunzi 21 waliokolewa na watatu hawakuonekana lakini saa chache baadaye, miili mitatu iliopolewa. Ajali hiyo ilitokea jana saa 10 alasiri.  Mkuu wa Wilaya ya Geita, Herman Kapufi amesema wanafunzi hao walikuwa kwenye mtumbwi waliotumia kuvuka wakitoka shuleni.
Powered by Blogger.