Trending News>>

MKUU wa Wilaya Mdogo Kuliko wote Tanzania na Sifa za Mwanaume Anayetamani Kuolewa naye

Zainab Abdallah, Mkuu wa wilaya ya Pangani ndiye kiongozi wa nafasi hiyo mwenye umri mdogo kuliko wote Tanzania, kwa sasa Zainab ana miaka 23 tu na bado hajaolewa lakini pia anazo sifa anazohitaji kutoka kwa mwanaume anayetamani kuolewa nae.

AYO TV na millardayo.com imempata Zainab Abdallah kwenye Exclusive na ameeleza jinsi anavyokutana na maswali mengi kuhusu lini ataolewa, nani ataolewa naye na je atakuwa na sifa zipi ili waendane.

“Nahisi nahitaji kuolewa na hata baadhi ya viongozi wameniambia Zainab utafika mbali sana lakini una mtihani mmoja tu unahitaji kuolewa, hilo ndio swali kubwa naulizwa. Unajua mimi ni binti mdogo lakini nimepanda sana kwenye siasa.”

“Kuna wakati nafikiria kuolewa na mwanaume ambaye hayuko kabisa kwenye masuala ya siasa, kwasababu tutaweza kuiweka sawa familia wakati mimi napokuwa kwenye kazi yeye atakuwa na muda na watoto, wakati mimi niko na watoto yeye atakuwa kwenye siasa, mwanaume ambaye ni mfanyabiashara labda au meneja wa taasisi fulani tena akiwa hajulikani nitakuwa salama zaidi” – Zainab Abdallah (DC Pangani) VIDEO: 


No comments:

Powered by Blogger.