KRC Genk ya Samatta imepoteza mchezo dhidi ya Zulte-Waregem
Ligi Kuu soka Ubelgiji iliendelea usiku wa December 21 2016 kwa michezo kadhaa kuchezwa, timu ya KRC Genk inayochezewa na mtanzania Mbwana Samatta ilikuwa mgeni wa timu ya Zulte-Waregem katika uwanja wa Regenboog.
KRC Genk ikiwa ugenini imekubali kupoteza mchezo kwa goli 1-0, goli ambalo lilifungwa na Souahilo Meite dakika ya 26 ya mchezo, kwa matokeo hayo KRC Genk wanakuwa na takwimu kwa mechi zao 5 zilizopita kushinda mechi 2, kufungwa mechi 2 na kutoka sare mchezo mmoja.
Kwa upande wa Mbwana Samatta kocha wake Peter Maes ameendelea kumuamini na kumpanga kwa dakika zote 90, mchezo uliyopita Genk walilazimishwa sare ya kufungana goli 2-2 na Standard de Liege goli la pili la kusawazisha la Genk lilifungwa na Mbwana Samatta dakika ya 78.

No comments:
Post a Comment