HIZI NDIO DAWA ZA HOSPITALINI ZINAZOUA NGUVU ZA KIUME
Dawa zote zinazopatikana mahospitalini na maduka ya madawa zinaletwa kusaidia watu wenye matatizo mbalimbali, japokua baadhi ya dawa hizo huambatana na madhara madogo na makubwa kwenye mwili wa binadamu. madhara madogo madogo huweza kua kichefuchefu,kizunguzungu, kutapika, kuharisha na kadhalika. na madhara makubwa huweza kua kansa, madonda ya tumbo, ugumba, kuishiwa nguvu za kiume na kadhalika. leo ntaenda kuongelea dawa za hospitalini ambazo zinhusika sana kuua nguvu za kiume na kama una tatizo hili uziepuke mara moja.
Dawa za kutibu presha; kuna dawa nyingi sana za kutibu presha na hufanya kazi kwa njia tofauti tofauti yaani ikishindwa hii unapewa nyingine na zifuatazo ni baadhi ambazo huua nguvu za kiume. mfano Hydrochlorothiazide, Hydropres, Inderide, Moduretic, Oretic, Lotensin, Chlorthalidone (Hygroton), Triamterene (Maxide, Dyazide), Furosemide (Lasix), Bumetanide (Bumex), Guanfacine (Tenex), Methyldopa (Aldomet), Clonidine (Catapres), Verapamil (Calan, Isoptin, Verelan) Nifedipine (Adalat, Procardia), Hydralazine (Apresoline), Captopril (Capoten), Enalapril (Vasotec), Metoprolol (Lopressor), Propranolol (Inderal), Labetalol (Normodyne), Atenolol (Tenormin), Phenoxybenzamine (Dibenzyline), Spironolactone (Aldactone).
Dawa za kutibu kifafa, msongo wa mawazo na wasiwasi; hizi hupewa kwa wagonjwa wenye msongo wa mawazo na kifafa. mara nyingi huleta uzingizi na kumfanya mtu aapate nafuu lakini pia dawa hizo hupunguza nguvu za kiume.mfano Fluoxetine (Prozac), Tranylcypromine (Parnate), Sertraline (Zoloft) Isocarboxazid (Marplan), Amitriptyline (Elavil), Amoxipine (Asendin), Clomipramine (Anafranil) Desipramine (Norpramin), Nortriptyline (Pamelor), Phenelzine (Nardil), Buspirone (Buspar), Chlordiazepoxide (Librium),Clorazepate (Tranxene),Diazepam (Valium)
Doxepin (Sinequan), Imipramine (Tofranil), Lorazepam (Ativan), Oxazepam (Serax), Phenytoin (Dilantin).
Dawa za kutibu matatizo ya aleji; hizi ni dawa amazo mara nyingi hutumika kutibu mafua, miwasho, kutetemeka mwili,kuzuia kutapiaka na kadhalika lakini huua nguvu za kiume taratinu mfano Dimehydrinate (Dramamine), Diphenhydramine (Benadryl), Hydroxyzine (Vistaril), Meclizine (Antivert), Promethazine (Phenergan).
Dawa za maumivu; hizi ni dawa ambazo hutumika kutibu maumivu makali ya mwili kama jointi, mgongo, miguu na kadhalika lakini bahati mbaya huacha sehemu nyeti katika halia ambayo sio nzuri mfano Naproxen (Anaprox, Naprelan, Naprosyn) na Indomethacin (Indocin).
Dawa za kutibu madonda ya tumbo; hutumika na watu wengi sana kuponya na kuondoa maumivu makali yanayosababishwa na madonda ya tumbo lakini huacha madhara hayo.mfano cimetidine, Nizatidine (Axid), ranitidine (Zantac).
Dawa za kutibu tezi dume; pamoja ya kua tezi dume hutibiwa moja kwa moja kwa upasuaji lakini kuna dawa ambazo mgonjwa anapewa kabla ya kufikia hatu ya kupasua na pia dawa hizi humpunguzia makali ya ugonjwa.mfano flutamide(Eulexin), leuprolide (Lupron)
dawa za kutibu kansa; dawa hizi hazipatikani madukani kabisa, na hutolewa kwenye hospitali maalumu kama ocean road, dar es laam kupunguza makali ya ugonjwa wa kansa. mfano wa dawa hizo ni Flutamide (Eulexin), Leuprolide (Lupron).
Dawa za moyo; hizi ni dawa amabazo hutumika kutibu watu wenye matatizo ya moyo.. mara nyingi dawa hii hupewa kwa watu ambao mioyo yao haisukumi damu vizuri.mfano norpace.
Mwisho; kama una tatizo la kupungukiwa nguvu za kiume na unaatumia baadhi ya dawa hizi, basi ongea na daktari wako anayekutibu akubadilishie dawa. ni hatari kufanya maamuzi mwenyewe bila kumshirikisha daktari. nguvu za kiume ni nzuri lakini maisha ni matamu zaidi.
No comments:
Post a Comment