Trending News>>

Athari za kiafya za vyakula vyenye Wanga


MOJA ya vyakula ambavyo tumekuwa tukitumia kwa wingi hasa Watanzania wenye kipato cha kati na chini kabisa ni vyakula vya aina kuu tatu, Wanga, Protini na Mafuta (Fats).

Na kwa kiwango kidogo sana tunatumia vitamin na madini katika milo yetu. Moja ya masomo ya chakula tunayofundishwa ni kula mlo kamili.Watu wengi tumekuwa tukitumia elimu hiyo hadi hapa tulipofika.

Napenda kusema tu kwamba mlo kamili ni kwa ajili ya mtu mzima ambaye hana ugonjwa wowote na ni kwa yule tu ambaye hataki kula kiafya.

Napenda kusema haya kwa sababu tumekuwa tukila vyakula vya namna ile ile lakini tumekuwa tukiugua mno magonjwa mbalimbali yatokanayo na lishe mbovu. Hadi sasa ugonjwa wa kisukari hapa duniani unaua zaidi ya ugonjwa wa UKIMWI, swali la kujiuliza je, tumejitenga wapi mbali katika lishe?

Leo nataka nikueleze kidogo kuhusu sayansi ya chakula aina ya wanga. Maana kila mtu ninayemwelekeza njia sahihi ya kupunguza uzito anakwambia nitaishije bila chakula cha wanga? Mwili wako hutumia vyakula vikuu aina tatu ambavyo ni wanga, protini na mafuta.

Na unatakiwa ujue kuwa gramu moja ya wanga hutengeneza nishati ya mwili kalori nne, ambapo protini nayo hutengeneza kalori nne na Fats hutengeneza kalori tisa. Unaona ni zaidi ya mara mbili ya nishati zinazotengenezwa na chakula cha wanga.

Hii ina maana kuwa ninaposema kuwa tunaweza kupunguza wanga na ukaishi ukiwa na nguvu nyingi zaidi hata ya ulivyo kuwa katika lishe ya wanga nyingi.

KWA NINI NAKUSHAURI UPUNGUZE WANGA KIAFYA?

Unapokuwa umepunguza wanga au kuacha kabisa ulaji wa vyakula vyenye wanga nyingi, mfano mikate, ugali, wali na tambi. Hakikisha kitendo hicho kiendane na kuongeza kiwango cha mafuta na vyakula vya protini mwilini mwako katika lishe yako. Hii itaufanya mwili wako kuanza kutumia mafuta kama nishati ya mwili ya kwanza kujitengenezea nguvu.

Viungo vya binadamu kama ini na figo vinapokuwa vinatumia mafuta kuzalisha nishati ya mwili hutengeneza viini vya nishati viitwavyo Ketone Bodies, ambavyo hivi ndivyo hutumiwa na seli za mwili kujitengenezea nishati kwa wingi.

Hivyo basi, unapokuwa unajizuia kutumia vyakula vya wanga mwili wako utatumia karibia siku tano hadi wiki kuanza kutumia mafuta kama nishati ya mwili na hicho kitendo tunaita Keto Adaption.

Ningependa kusema kwamba Keto Adaption ni ile hali ya mwili wako kujenga mazoea ya kutumia mafuta kama chanzo cha nishati ya mwili na hapo ndipo utaanza kuona mabadiliko katika mwili wako makubwa.

Utakuwa unajisikia mwenye nguvu na unatashangaaa dalili mbalimbali zilizokuwa zinakusumbua zinapotea hii ni kwa sababu ya uwezo mkubwa wa ketone bodies katika mwili wako dhidi ya glucose.

Sote tunajua kwamba ulaji wa vyakula vya wanga kwa wingi na vyakula vyenye sukari nyingi vinaongeza kiwango cha sukari kwenye damu zaidi ya kiwango ambacho mwili wako unaweza kuhimili.

Mfano; kiwango cha kawaida cha sukari kinachohitajika mwilini mwako ni kijiko kimoja cha chai, hiki ni kiwango ambacho hakiwezi kukuletea matatizo. Basi kama binadamu anaishi kwa sukari inayokadiriwa kuwapo kwenye damu kama kijiko kimoja tu cha chai.

Unywaji wa soda moja unaweza kuongeza zaidi ya vijiko 10, hivyo basi mwili wako unakuwa unashindwa kuhimili sukari iliyozidi.

Kwa wale wanaopenda kula baga, inakadiliwa kuwa baga moja ya kati inaweza kutoa sukari zaidi ya vijiko 16 kwenye damu.

Swali la kujiuliza mwili unapeleka wapi sukari iliyozidi wakati miili yetu inahitaji sukari kiwango kidogo kama kijiko kimoja tu kuishi?
Mwili hutengeneza maji kutoka kwenye seli za kongosho ziitwazo beta seli, maji haya ni homon iitwayo Insulin, kazi kubwa ya insulin ni kutunza glucose hii katika damu kwa matumizi ya baadae, na inatunza katika kiasi maalumu katika mfumo wa Glycogen na kiasi kikubwa katika mafuta.

Hivyo basi, mafuta haya huhifadhiwa katika sehemu mbalimbali kama tumboni, shingoni, mikononi, kifuani na kiunoni. Mafuta haya huhifadhiwa katika mfumo wa Tryglycerides ambayo haya ni miongoni ya mafuta mabaya mwilini mwako.

Sasa mtu anayekwambia wanga nyingi katika chakula chako ni salama anakudanganya kwa kiasi kikubwa kwani tunaona jinsi gani ulaji wa kiwango kingi cha vyakula vya wanga na sukari vinavyosababisha sukari kupanda kupita kiasi na insulin kuanza kuhifadhi katika mafuta.

Kila siku nasema, tumekaririshwa adui mkuu ni fats na kujisahau ulaji mbovu wa vyakula vya wanga huku tukiishia kulea vitambi na magonjwa sugu, hii yote ni kutokuwa na ufuatiliaji wa lishe nzuri na salama kwako.

MADHARA MENGINE YA SUKARI
Napenda kuwarudisha nyuma kidogo katika somo la bailojia. Tulijifunza kuwa miili yetu imejengwa kwa kiini kidogo sana kiitwacho seli ambapo shughuli zote za mwili zinafanyika humo.

Nilijifunza kuwa ndani ya seli kuna viungo vidogo vidogo navifananisha na (Apartments kwenye nyumba kubwa) moja wapo ni Mitochondria, hiki ni kiungo kidogo katika seli ambacho kinahusika na kuzalisha nishati ya mwili tu. Pia nikikumbuka watu wote tulijifunza kwamba mwili wetu hujitenegenezea nishati ya mwili au nguvu kupitia kuifanyia kazi sukari iliyo ndani ya damu baada ya kuingia ndani ya seli.

Hivyo basi insulin ni kama ufunguo ambao unafungua milango ili sukari iweze kuingia ndani ya seli hadi kwenye mitochondria. Mwili wako unapokuwa unatumia hewa ya oxygen kuna uwezekano mkubwa wa kupatikana kwa athari iitwayo Oxdative stress.

Hii ndiyo inayofanya chuma kipate kutu, hii ndiyo inayofanya mafuta ukiyaweka kwenye jua kwa muda mrefu yanaharibika. Basi mwili wako unakuwa unatengeneza vihatarishi viitwavyo Reactive Oxygen Species kwa kifupi huitwa Free Radicals.

Hizi ni sumu ambazo hupatikana wakati mwili unajitenegenezea nishati yake kwa kutumia oxygen na hizi zinapokuwa kiwango kikubwa huweza kuharibu kabisa seli na kuziua na pia zinaweza kupelekea kupata magonjwa sugu kama saratani.

Hivyo, tafiti zinaonesha kwamba vyakula vya wanga na sukari vina matokeo makubwa ya kutenegeneza Free Radicals nyingi kupita kiasi.

Miili yetu ina kiwango fulani cha viondoa sumu ambavyo vinaipunguza sumu ya free radicals kuepusha kusababisha magonjwa kwa kuziua seli.

Lakini panapokuwa na kiwango kikubwa cha uzalishaji wa free radicals mwili unashindwa kuhimili na hatimaye free radicals zinaanza kuleta madhara mwilini mwako. Kadri mitochondria zinavyodhoofika ndivyo magonjwa nyemelezi ya lishe yanavyotukabili kila kukicha.

No comments:

Powered by Blogger.