Trending News>>

Ligi ya Vijana U-20 Tanzania Bara- Kagera Sugar vs Yanga hakuna mbabe


Pazia la Ligi ya Vijana U-20 ya Timu zinazoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara limefunguliwa leo ambapo Kagera Sugar walikuwa wenyeji dhidi ya Yanga na mchezo kumalizika kwa sare ya bao 1-1 katika mchezo uliofanyika kunako Uwanja wa Kaitaba mkoani Kagera.

Katika mchezo huo ambao mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Mkoa huo Meja Jenarali Mstaafu Salum Kijuu, timu zote zilimaliza kipindi cha kwanza bila ya kufungana huku mchezo ukiwa na msisimko mkubwa.

Katika kipindi cha pili Yanga walifanikiwa kufungua lango la Kagera kwa kufunga bao safi kupitia kwa Yusuf Anthony Mhilu dakika ya 68 baada ya kuunganisha mpira wa adhabu ndogo.

Hata hivyo bao hilo halikuwazuia Kagera Sugar kufanya mipango yao na ndipo mnamo dakika ya 90 mchezaji Christopher Pascal alipofanikiwa kuisawazishia Kagera bao baada ya kutumia vizuri udhaifu wa mabeki wa Yanga.

No comments:

Powered by Blogger.