Trending News>>

American dream ya Steven Gerrard imefeli


Hatimaye Steven Gerrard ametangaza rasmi kumalizana kucheza soka kwenye ligi ya marekani alivyokua na club ya L.A Galaxy. Liverpool icon ametangaza rasmi kwamba kwa sasa basi tena kucheza kwenye club hiyo ambao amefunga jumla ya magoli 5, akitoa assist 14 na kucheza mechi mara 34 ndani ya miezi 18.

Mchezaji huyu wa zamani wa Liverpool alikua na ndoto za kufika Marekani na kushinda taji la ligi hiyo ya soka. Lakini baada ya kucheza kote ameshindwa kutimiza ndoto hizo.. Gerrard amesema, “Nilivyokuja hapa L.A nilikua na ndoto na malengo ya kusaidia club hii kushinda taji lingine kwenye ligi. Najiskia vibaya sijafanikisha hilo ambalo lilikua lengo langu lakin nikiangalia nyumba nafurahia yote tuliyofanikisha. Tumeweza kucheza hadi hatua ya mtoano mara mbili mfululizo na kumbu kumbu nyingine nyingi uwanjani”.

Steven Gerrard sio mchezaji pekee kutoka England kumalizana na ligi hiyo. Mchezaji mwingine ni wa New York City Frank Lampard ambae ameondoka wiki iliyoita.

No comments:

Powered by Blogger.