Trending News>>

MAKAMU WA RAIS MHE.SAMIA SULUHU AZINDUA KAMPENI YA UCHUNGUZI WA SARATANI YA MATITI NA YA MLANGO WA KIZAZI KATIKA MKOA WA MWANZA



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu  Hassan akihutubia wakati wa uzinduzi wa kampeni ya uchunguzi wa saratani ya matiti pamoja na ya mlango wa kizazi kwenye uwanja wa Furahisha jijini Mwanza. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu  Hassan akizungumza na Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalim (katikati) pamoja na Mwenyekiti wa Chama cha Madaktari Wanawake Tanzania Dk. Serafina Mkuwa wakati wa uzinduzi wa kampeni ya uchunguzi wa saratani ya matiti pamoja na ya mlango wa kizazi kwenye uwanja wa Furahisha jijini Mwanza. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu  Hassan akimsikiliza Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalim kwenye moja ya mabanda yaliokuwa yanatoa huduma wakati wa uzinduzi wa kampeni ya uchunguzi wa saratani ya matiti pamoja na ya mlango wa kizazi kwenye uwanja wa Furahisha jijini Mwanza. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu  Hassan akiwapungia mkono wananchi waliojitokeza wakati wa uzinduzi wa kampeni ya uchunguzi wa saratani ya matiti pamoja na ya mlango wa uzazi kwenye uwanja wa Furahisha jijini Mwanza. 
Sehemu ya Wanawake waliojitokeza kwennye uzinduzi huo.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewahakikishia wananchi kuwa serikali imeweka mipango na mikakati thabiti ya kukabiliana na idadi kubwa ya vifo vinasababishwa na saratani hasa saratani ya matiti na mlango wa kizazi kote nchini.

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo katika viwanja vya furahisha jijini Mwanza wakati akizundua kampeni ya uchunguzi wa saratani ya matiti na mabadiliko ya awali ya saratani ya mlango wa kizazi mkoani humo.

Katika hotuba yake kwa mamia ya wananchi wa mkoa wa Mwanza waliojitokeza katika uzinduzi huo, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amesema Tanzania ikiwa ni nchi mojawapo Kusini mwa Jangwa la Sahara ina kiwango cha juu cha vifo vya saratani ya matiti na mlango wa kizazi ambapo asilimia 60 ya vifo vyote vinavyotokea Kusini mwa jangwa la Sahara vinasababishwa na saratani hiyo.

Makamu wa Rais amesema kuwa vifo vingi vinatokana na uelewa mdogo, imani potofu,gharama kubwa za matibabu,unyanyapaa na kuwepo kwa vituo vichache wa kufanyia uchunguzi hapa nchini ambapo kwa sasa tiba ya mionzi inapatikana katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Roas, Dar es Salaam.

Katika kukabiliana na tatizo hilo, Makamu wa Rais amesema kuwa Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto imepokea kiasi cha shilingi bilioni Tano kutoka Benki ya Dunia fedha ambazo zitawezesha vituo Vitatu kwa kila Halmashauri ambavyo vitasaidia kuboresha huduma za uchunguzi na matibabu ya mapema ili wanawake kote nchini hasa wale wale wa vijijini waweze kupata huduma hizo kwa urahisi na kwa ukaribu kwenye maeneo wanayoishi.



“Wote ni mashuhuda kwa namna saratani ya mlango wa kizazi inavyosababisha vifo vingi hali ambayo hutokana na magonjwa wanaogundulika na ugonjwa kuwa tayari wamefikia hatua isiyotibika na kwa pamoja saratani hizi mbili husababisha zaidi ya asilimia 50 ya vifo vyote vya akinamama”

Makamu wa Rais amesisitiza kuwa kwa sasa tayari kuna vituo takribani 300  vinavyotoa huduma za upimaji wa dalili za awali katika vituo vya afya kote nchini na hivyo vituo vipya vitaongeza huduma endelevu ili kupunguza vifo vitokanavyo na saratani.

Makamu wa Rais pia ametoa wito maalum kwa wanaume kote nchi kuunga mkono kampeni hiyo kwa kuwaruhusu wanawake na wasichana kwenda kupima saratani hiyo na amewapongeza na kuwashukuru wanaume wa mkoa wa Mwanza kwa kuwasindika wake zao na watoto wao wa kike kwenda kwenye vituo vya afya kwa ajili ya kupima saratani hiyo na kupatiwa tiba.

Makamu wa Rais amepongeza Chama cha Madaktari Wanawake Tanzania- MEWATA na wadau wote kwa kuanda zoezi la huduma za uchunguzi wa dalili za awali za saratani ya mlango wa kizazi.

Kwa upande wake, Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amesema kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi zenye wagonjwa wengi wa saratani ya mlango wa kizazi na pia ndiyo inaongoza katika nchi za Afrika mashariki.

Amesema kuwa idadi ya wanawake 6241 hugundulika kuwa na saratani kila mwaka na kati yao zaidi ya nusu yaani 4355 hufariki dunia.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

No comments:

Powered by Blogger.