Model maarufu wa Bongo alitosa kutokea kwenye video ya Salome, alidai six figures, Diamond akamchomolea
Kuna model maarufu wa Bongo aliyetosa kuonekana kwenye video ya wimbo wa Diamond ‘Salome.’
Model huyo anadaiwa kutaka alipwe fedha nyingi ambazo zilikuwa nje ya bajeti ya staa huyo.
“Bajeti yangu haikuweza kumuafford, na siwezi kufanya kitu kimashauzi wakati bajeti yangu ndogo,” Diamond alikiambia kipindi cha The Playlist cha Times.
Diamond anasema alichokikosa model huyo baada ya kukataa kufanya video hiyo si fedha tu, bali exposure ambayo angeipata baada ya hapo.
“Si uchawi, sio uongo, sio ushirikina, unavyofanya video na mimi unakuwa mkubwa na inakuongezea dau,” alisisitiza kwa kuongeza kuwa watu kibao humuomba waonekane kwenye video zake bure lakini hukataa kwakuwa ni lazima awalipe.
Diamond amedai hiyo ndio sababu hatokuja kulitaja jina lake kwakuwa atampa kiki na atakuwa mkubwa.
“Nilimuambia, angalia angle zote mbili, angalia kwamba nakulipa kiasi lakini kushiriki kwako kwenye hii video itakuongezea ukubwa zaidi, itakupa biashara nyingi.”
Alitoa mfano kuwa show nyingi za MTV alizowahi kutumbuiza alifanya bure kwasababu alizitumia kukuza jina lake. Anasema wakati mwingine hadi dancers huwasafirisha kwa gharama zake mwenyewe.
“Lakini najua show ninayoifanya pale ikitoka itanipa hela nyingi baadaye. Niliheshimu alichokisema ndio maana sikumind, nilisema naheshimu sababu umejitambua na umeona thamani yako ni nini, lakini bahati mbaya sisi bajeti yetu haikufika huko.”
No comments:
Post a Comment